Oscar Oscar dharau zako kwa Simba hazivumiliki

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
FB_IMG_1683484997610.jpg

Kuwa kwako Mwandishi wa habari kusikung'oe ubongo .

Hivi Simba hii hukuwahi kuiona ?

FB_IMG_1683492164750.jpg

Heshima ni kitu cha bure ukae ukijua hilo .

Pamoja na umuhimu wa Katiba mpya lakini huku ulikoenda siko
 
wanathiimba wenzangu, tukubali tu, tujipange kwa msimu ujao, takataka nyingi saana za kuondolewa simba, eneo la katikati limechoka, ukweli ambao watu wanaukataa kila siku, midfilder zetu zipo zipo tu, usahihi wa pasi mdogo, akipiga pasi 10, 5 anapatia 5 anakosea na katika hizo 5 hakuna ya kushambulia ni changamoto kwa kweli, niliwahi kusema msimu upo mwanzoni, tunashinda kwa sababu ya uwezo binafsi wa kina chama na phiri pale mbele.
Bado hatuna midfild wa ziada benchi, benchi letu nafasi ya midfild huwa kama hakuna mtu, hawazidi wawili, wengine kiasili ni mabeki..
Benchi yupo boko,sakho,banda, kenedy, nyoni nafasi za mbele ni wengi, hivyo midfild zetu uchwara zikifeli tu, hakuna namna inabidi azike babu erasto au mkude(morali yake ya upambanaji imeshuka)
Kale ka nelson okwa tulikadharau ila ni kamidfild kisheti, kanapiga pasi anafatilia pasi yake, anaugawa uwanja, anatembea na timu, anapiga pasi za kumiliki mpira(kusambaza upendo), anapiga pasi za mashambulizi, bahati mbaya walikuwa wanampanga namba 10 ufanisi wake ukawa mdogo, nasi pia viongozi uvumilivu hawana, mwishowe akaja sawadogo, bora ya mimi nisiye na mazoezi kuliko sawa dogo mwenye mazoezi

Jingine hivi phiri hajapona majeruhi au kakosea nini hasa, yaani kocha anaona boko bora kuzidi... staajabu ya musa uone ya firaauni.
 
Mbona kawaida tu. Ushabiki wa soka tusiuwekee sana kipaumbele kiasi cha kufikia kuumizwa na utani utani kutoka huku na huko. Hakuna sababu ya kuumia maana kuna nyakati ulifurahi pia. Soka iwe sehemu tu ya burudani, lakini tuwekeze zaidi katika maisha yetu na ya vizazi vyetu
 
Mara moja, maana nimetoa comment moja.
Kama ni mara moja si walishatupia au hukuona? Na kama vipi ingia tu google u-search Gazeti la Mwananchi:Fainali ya kombe la CAF 1993 kati Simba vs Stella Abdijan. Utaona picha ya Mhe.Prof.Philemon Sarungi akimvisha medali mchezaji wa Simba Damian Kimti.

Lakini pia katika kusearch kwako utakutana na maelezo ya mchezaji Malota Soma akitaja kuwa, siku hiyo ya fainali Simba waliambulia medali ya fedha, na pia mfadhili wao (Azim Dewji) aliwapa kifuta jasho cha magari ya Corola kila mchezaji.
 
wanathiimba wenzangu, tukubali tu, tujipange kwa msimu ujao, takataka nyingi saana za kuondolewa simba, eneo la katikati limechoka, ukweli ambao watu wanaukataa kila siku, midfilder zetu zipo zipo tu, usahihi wa pasi mdogo, akipiga pasi 10, 5 anapatia 5 anakosea na katika hizo 5 hakuna ya kushambulia ni changamoto kwa kweli, niliwahi kusema msimu upo mwanzoni, tunashinda kwa sababu ya uwezo binafsi wa kina chama na phiri pale mbele.
Bado hatuna midfild wa ziada benchi, benchi letu nafasi ya midfild huwa kama hakuna mtu, hawazidi wawili, wengine kiasili ni mabeki..
Benchi yupo boko,sakho,banda, kenedy, nyoni nafasi za mbele ni wengi, hivyo midfild zetu uchwara zikifeli tu, hakuna namna inabidi azike babu erasto au mkude(morali yake ya upambanaji imeshuka)
Kale ka nelson okwa tulikadharau ila ni kamidfild kisheti, kanapiga pasi anafatilia pasi yake, anaugawa uwanja, anatembea na timu, anapiga pasi za kumiliki mpira(kusambaza upendo), anapiga pasi za mashambulizi, bahati mbaya walikuwa wanampanga namba 10 ufanisi wake ukawa mdogo, nasi pia viongozi uvumilivu hawana, mwishowe akaja sawadogo, bora ya mimi nisiye na mazoezi kuliko sawa dogo mwenye mazoezi

Jingine hivi phiri hajapona majeruhi au kakosea nini hasa, yaani kocha anaona boko bora kuzidi... staajabu ya musa uone ya firaauni.
Kolo umejielezea sana🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom