Oscar Oscar na Masoud si sawa kumsakama Jeff

Oscar Oscar na Masoud si sawa kumsakama Jeff

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Nimetokea kuwa msikilizaji wa Radio ya E-FM hasa kipindi cha michezo kuanzia saa tatu asubuhi.

Hii imetokana na umahiri wa uchambuzi wa soka hasa wa Jemedari Said Kazumari angeongezeka na Amri Kiemba kipindi kingekosa mpinzani kabisa.

Leo ni mara ya pili hivo hawa Oscar na Masoud wanatokea kumsakama Jeff-english katika maoni yake.

Katika maoni yake kwa maoni ya mchezaji Abdi Banda kufuatia mechi ya Mtibwa na Simba msimu huu. Wao wamemkatisha asitoe mifano ya misimu iliyopita ilhali wao wametoa mechi za Simba walizocheza msimu huu huu.

Muacheni Jeff-english atoe alichonacho tumsikie.
 
Hapo hamna wachambuzi, wote hao wanaongekea siasa ya mpira wanaochambua mpira technically ni Ambagile w wasafi, Ally Kamwe na Ally mayai wa azam wengine hawawezi.
Ambangile ndio yule anaependa kuingiza maneno mawili matatu ya kiingereza...basi.. sentenso haitimii... ndio mchambuzi wetu huyo.
 
Ambangile ndio yule anaependa kuingiza maneno mawili matatu ya kiingereza...basi.. sentenso haitimii... ndio mchambuzi wetu huyo.
Well.
Ambangile udhaifu wake ni uoga wa kutamka msimamo wa anachoamini. Mara nyingi anataka awe upande salama kwa kufuata ngoma ya mashabiki. Huwa nampenda Edo Kumwembe, haangalii usalama wake, anatamka anachoamini hata kama kitawaudhi baadhi au upande mmoja
 
Ambangile ni mwoga wa kupigwa mawe hasa na simba na yanga so hujitahidi kubalance na hapo ndiyo anapokosea..eddo na dauda wao kama ni nyeusi ni nyeusi hawaogopi chochote.kihemba na jemedari nao wako vizuri hawajali mihemko ya vilabu vya kariakoo kama wamezingua huwaambia ukweli
 
Hapo hamna wachambuzi, wote hao wanaongekea siasa ya mpira wanaochambua mpira technically ni Ambagile w wasafi, Ally Kamwe na Ally Mayayi wa azam wengine hawawezi.
Sikuvutiwa na Wasafi FM kwa uwepo wa Maulidi Kitenge na imekuwa bahati mbaya karejea E FM. Sina ujanja.
 
Back
Top Bottom