JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Jua ni muhimu katika uzalishaji wa Homoni ya Melatonin ambayo hudhibiti mzunguko wa usingizi.
Inaelezwa kuwa jinsi mwili wako unavyoweza kuzalisha Melatonin za kutosha ndivyo mfumo wako wa usingizi unavyoimarika.
Pia mwanga wa jua huchochea seli kwenye ngozi na kuzalisha Vitamin D inayoboresha afya ya mifupa na meno na kumkinga mtu na hatari ya kushambuliwa na magonjwa ya moyo, kisukari na saratani na magonjwa ya kuambukizwa.
Umuhimu mwingine wa jua hasa la asubuhi ni pamoja na kudhibiti msongo wa mawazo na kupunguza uzito.