Otango Osale ni nani huyu mtu?

Goodvision

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2012
Posts
858
Reaction score
467
Heshima mbele waikuu hapa JF. Tangu nikiwa mdogo na mpaka sasa nimemaliza miaka 3 sasa nasikia baadhi ya watu wakisimulia habari kuhusu mtu mmoja aitwaye Otango Osale, tafadhali wakuu mwenye historia yake atupie hapa tupate kumfahamu vizuri.
Nawasilisha
 
john tongo, OSALE OTANGO alikuwa mpigania uhuru (freedom fighter) kutoka mkoani Tanga kwenye miaka ya 1950. Baadaye alihama kutoka maeneo ya LUSHOTO akahamia Amboni TANGA na kwenye yale mapango ndipo walipokuwa wanajificha. ENDELEA KUTAFITI MKUU.
 
Last edited by a moderator:
Alikuwa na msaidizi wake Paulo, walikosea masharti
 
Asante kwa taarifa wakuu nitaendelea kudadisi taarifa zaidi
 
alikuwa na msaidizi wake Paulo, walikosea masharti

Walikuwa wawili Osale Otango na Paul, waliwasumbua sana Wazungu, kwa mfano; walikua na uwezo wa kuwaambia kabisa Wazungu kuwa watakula nao chakula cha mchana, na hivyo wazungu huweka mitego yote ili wawakamate lakini at the agreed time jamaa wanafika wanakula na kufanya wanavyotaka bila ufahamu wa Wazungu. Wakishaondoka tu Ndio jamaa wanastuka
 
Ngoja mzee wa historia sheikh Mohamed Said atakupa mpaka majina ya wake zao yule jamaa namkubali ni soo
 
Last edited by a moderator:
Wote inasemekana walikufa lakini hawakushikwa ndio maelezo yakiyokuwepo tulipokuwa wadogo miaka ya 90 tuliyopewa kule
 
Walikufa kwa kutofuata maekekezo, walikatazwa kabisa wasije wakawagegeda wazungu! Jamaa wakanogewa na mchezo wao wa kuwachezea wazungu wakajikuta wanataka papuchi za kizungu
 
Inaonekana kuna historia nzuri sana kuwahusu watu hawa,
Tafadhali wenye info za kutosha karibuni sana mtiririke hapa jamvini.
cc. mohamed said
 
It is a very interesting story jinsi Huyu Mgosi alivyowasumbua Wazungu
 
Miaka mingi kidogo nakumbuka Daily News walitoa makala ndefu kuhusu huyu bwana.Na kama sikosei ni kuwa alipigwa risasi na askari wa Kikoloni.
 
mkuu

Alikuwa na asili ya kenya.......alikuja Tanga kwa ajili ya kufanyakazi katika mashamba ya mkonge.....alifungwa (kosa nimesahau).....alitoroka gerezani korogwe.. waliwasumbua sana wazungu akiwa na Paul.....walipiga sana matukio...in short Tanga yote ilkuwa chungu kwa wazungu.....inadaiwa walipewa dawa sharti ilikuwa wasifanye tendo la ndoa na wanawake wa kizungu.....ukizingatia kwamba jamaa walikuwa wana uwezo wa kuingia ndani ya nyumba na kuondoka bila wazungu kujua.....maficho yao yalkuwa mapango ya amboni ......jeshi la polisi la kikoloni waliwashindwa ilibidi sniper (mdunguaji)kutoka uingereza aletwe.....sasa siku Osale alikuwa anatoka kula bata (disko) Korogwe/Lushoto (sina uhakika) mdunguaji huyo naye alikuwepo eneo la tukio ......jamaa walikuwa kwenye kundi ....mzungu ili kumtambua akaita Osaleeee......ile kugeuka tu...akala shaba (risasi) kazaa huo ndo ukawa mwisho wake.....

mwisho wa Paul nimeusahau subiri nichimbechimbe.........

inadaiwa jamaa mwisho wao ulitokana na kungonoka na demu wa kizungu lakini tetesi zingine zinasema baadhi baadhi ya wazee walitoa siri yao kwa wazungu.....

NB. ukitaka full story nenda mapango ya Amboni
 
Hivi mnaposema waliwasumbua wazungu ni serious kweli? hilo tu kutaka kungonoka na maadui ni udhaifu kwenye harakati.
C.C Elli
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…