mkuu
Alikuwa na asili ya kenya.......alikuja Tanga kwa ajili ya kufanyakazi katika mashamba ya mkonge.....alifungwa (kosa nimesahau).....alitoroka gerezani korogwe.. waliwasumbua sana wazungu akiwa na Paul.....walipiga sana matukio...in short Tanga yote ilkuwa chungu kwa wazungu.....inadaiwa walipewa dawa sharti ilikuwa wasifanye tendo la ndoa na wanawake wa kizungu.....ukizingatia kwamba jamaa walikuwa wana uwezo wa kuingia ndani ya nyumba na kuondoka bila wazungu kujua.....maficho yao yalkuwa mapango ya amboni ......jeshi la polisi la kikoloni waliwashindwa ilibidi sniper (mdunguaji)kutoka uingereza aletwe.....sasa siku Osale alikuwa anatoka kula bata (disko) Korogwe/Lushoto (sina uhakika) mdunguaji huyo naye alikuwepo eneo la tukio ......jamaa walikuwa kwenye kundi ....mzungu ili kumtambua akaita Osaleeee......ile kugeuka tu...akala shaba (risasi) kazaa huo ndo ukawa mwisho wake.....
mwisho wa Paul nimeusahau subiri nichimbechimbe.........
inadaiwa jamaa mwisho wao ulitokana na kungonoka na demu wa kizungu lakini tetesi zingine zinasema baadhi baadhi ya wazee walitoa siri yao kwa wazungu.....
NB. ukitaka full story nenda mapango ya Amboni