Othman: ACT Wazalendo itaingia SUK kama haya yametekelezwa

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
WhatsApp Image 2026-08-24 at 14.51.07.jpeg

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman, ametaja mambo matatu aliyosema yakitekelezwa ndipo kita kitaingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Mambo hayo pamoja na kuundwa kwa kamati ya pamoja yenye uwakilishi sawa kutoka vyama vilivyosaini makubaliano, kuundwa kwa tume ya pamoja ya kusimamia utekelezaji wa makubaliano hayo pamoja na kuweka utaratibu wa kuyaendeleza kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2030.

Kauli ya Othman imekuja tangu CCM na ACT Wazalendo walifikia makubaliano ya pamoja ya kisiasa Julai 9, 2026 ili kumaliza mkwamo wa kisiasa visiwani Zanzibar.

Soma pia: Zanzibar: CCM na ACT Wazalendo wafikia Maridhiano ya Kisiasa

WhatsApp Image 2026-08-24 at 14.51.05 (1).jpeg

Akizungumza katika mkutano wa wanachama Shangani, Mkoa wa Kaskazini, Wilaya ya Kaskazini A Unguja leo Agosti 24, 2026 Othman, alisema hatua ya kwanza kabla ya ACT Wazalendo kuingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni kuundwa kwa kamati ya pamoja yenye uwakilishi sawa kutoka vyama vilivyosaini makubaliano.

Othman ambaye ni Makamu wa Kwanza Mstaafu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar , aliongeza kuwa kamati hiyo itakuwa na jukumu la kuweka utaratibu wa utekelezaji wa mambo yaliyokubaliwa na kuainisha vipaumbele vya utekelezaji.

Othman alisema hatua nyingine ni kuundwa kwa tume ya pamoja ya kusimamia utekelezaji wa makubaliano hayo kwa mujibu wa sheria, pamoja na kuweka utaratibu wa kuyaendeleza kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2030.

“Baada ya hapo tutaenda kuungana na wenzetu katika kuendesha Serikali hiyo ili kuwaletea maendeleo Wazanzibari. Mambo mengine yatatekelezwa tukiwa serikalini kwa taratibu tutakazokubaliana,” alisema Othman.
WhatsApp Image 2026-08-24 at 14.51.05.jpeg

Alisisitiza kuwa ACT Wazalendo haikuingia katika makubaliano hayo kwa lengo la kutafuta vyeo, bali kwa ajili ya kutetea haki na maslahi ya Wazanzibari.

Othman alifafanua kuwa baada ya uchaguzi, chama hicho kilitakiwa kuwasilisha majina ya Makamu wa Kwanza wa Rais na mawaziri, lakini kilikataa kufanya hivyo kwa madai kuwa hakukuwa na uchaguzi.

“Lakini baada ya yote hayo tuliweka maslahi ya Zanzibar mbele, ndio tukakutana na wenzetu kutafuta maslahi ya wananchi wa Zanzibar,” alisema.

Alisema utekelezaji wa mambo yaliyokubaliwa unaweza kuisaidia Zanzibar kuvuka changamoto zake na kuleta maendeleo kwa wananchi, akisisitiza kuwa haiwezekani nchi yenye hadhi na heshima yake kuendelea kuwa katika mitafaruku ya kila siku.
WhatsApp Image 2026-08-24 at 14.51.06.jpeg

“Tungalikwenda kwenye makubaliano tukasema turejeshewe vitu vyetu vyote, tungalirejeshewa, je ndio tumerekesha tatizo? Hapana,” alisema.

Othman pia alisema ACT Wazalendo inaendelea kupigania kuondolewa kwa dhuluma ambazo zimechukua muda mrefu Zanzibar, ikiwemo kuhakikisha kuwa anayeshinda uchaguzi anatambuliwa na kutangazwa kuwa mshindi.

Alizitaja baadhi ya changamoto za utekelezaji wa makubaliano hayo kuwa ni wananchi kudhani kuwa makubaliano hayo ni ihsani kutoka CCM, badala ya kuyaona kama wito wa kitaifa unaolenga kutafuta maslahi mapana ya Zanzibar.

Aliwataka viongozi kusimamia na kudai utekelezaji wa makubaliano hayo kwa moyo mmoja bila unyonge, akisisitiza kuwa ni haki yao kudai mambo waliyokubaliana.

Othman pia aliwataka wanachama kutokata tamaa kutokana na watu wanaoweza kujaribu kuwakatisha moyo katika harakati za utekelezaji wa makubaliano hayo.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu, alisema hali ya maisha Zanzibar imeendelea kuwa ngumu kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.

“Lakini hakuna mtu anayeishi maisha ya raha kutokana na hali ngumu iliyozidi na kufanya raia kukosa hata mlo mmoja kwa siku,” alisema Jussa.

Alisema moja ya malengo ya makubaliano ya kutafuta umoja wa Wazanzibari ni kubadilisha maisha ya wananchi na kuwawezesha kuishi maisha yenye heshima.

Jussa alisema hakuna anayepaswa kuiachia Jumuiya ya Kimataifa jukumu la kuiweka Zanzibar katika hali inayostahili, bali wananchi wenyewe wana nafasi kubwa ya kutafuta mustakabali wa nchi yao.

“Hatuwezi kukata tamaa kwa sababu tunatafuta chetu ambacho ni haki yetu,” alisema.

Aidha, Jussa aliwataka viongozi wa ACT Wazalendo katika Mkoa wa Kaskazini A Unguja kuendelea kukiimarisha chama hicho, akikitaja kuwa ni jukwaa sahihi la kutafuta mabadiliko Zanzibar.

“Chombo hiki tukiimarishe na tukiendeleze, sababu kwanza tumeachiwa na Mzee wetu, marehemu Maalim Seif Sharif Hamad, na ndio chombo pekee cha kuivusha Zanzibar,” alisema Jussa.

Alisisitiza kuwa Wazanzibari hawapaswi kurudi nyuma katika kudai mamlaka kamili ya Zanzibar.

“Tusirudi nyuma katika kupigania mamlaka kamili ya nchi yetu ya Zanzibar na tusione haya kwenye hili, kwani haki yetu,” aliongeza.

Jussa alisema hatua zinazochukuliwa na ACT Wazalendo kupitia makubaliano hayo hazilengi Othman Masoud au yeye mwenyewe kupata nafasi binafsi, bali zinazingatia mustakabali wa Zanzibar na mamlaka yake.

“Leo upande wa pilitv tv wamekuwa wakali nao wanadai mamlaka kamili ya Tanganyika yao, sasa itakuwa wametufahamu,” alisema.

Aliwataka Wazanzibari kutorudi nyuma pale suala la Katiba litakapojadiliwa na kuendelea kusimamia wanachoamini kuwa ni haki na maslahi ya Zanzibar.

Kwa upande wake, Mwenyekiti Mstaafu wa ACT Wazalendo, Juma Duni Haji, aliwataka viongozi na wanachama wa chama hicho kutokata tamaa katika harakati za kupigania haki na maslahi ya Wazanzibari.

“Mtasikia mengi huko mitaani kuhusu yale tuliyosaini, tena ya kukatisha tamaa. Lakini tulieni mtusikilize sisi viongozi wenu,” alisema Duni.

Alisema makubaliano yaliyofikiwa hayakuangalia masuala ya vyeo, bali yalilenga heshima, umoja na maslahi ya Wazanzibari.
 
View attachment 3656136
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman, ametaja mambo matatu aliyosema yakitekelezwa ndipo kita kitaingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Mambo hayo pamoja na kuundwa kwa kamati ya pamoja yenye uwakilishi sawa kutoka vyama vilivyosaini makubaliano, kuundwa kwa tume ya pamoja ya kusimamia utekelezaji wa makubaliano hayo pamoja na kuweka utaratibu wa kuyaendeleza kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2030.

Kauli ya Othman imekuja tangu CCM na ACT Wazalendo walifikia makubaliano ya pamoja ya kisiasa Julai 9, 2026 ili kumaliza mkwamo wa kisiasa visiwani Zanzibar.

Soma pia: Zanzibar: CCM na ACT Wazalendo wafikia Maridhiano ya Kisiasa

View attachment 3656137

View attachment 3656138

View attachment 3656139

hakuna umuhimu.

Dr. Hussei Mwinyi anatosha kuiongoza Zanzibar na kuipaisha kiuchumi, kisiasa na kijamii.
hakuna wa kubabaika wala kupoteza muda na masharti useless kama hayo :1Head:
 
Waganga njaa
 
Back
Top Bottom