Aaaaahhh huu ni uwongo bwanaa....ni uwongo,kwahiyo TAKUKURU hawapo?yaani mtu upewe rushwa then uripoti ktk sehemu husika kisha ufungiwe maisha acha uwongo hapa hakuna mtoto mdogo,unalolisema haliwezekani hata kidogo, nikupe kisa kimoja...
Kuna jamaa aliomba rushwa kwa mtu ili amfanyie jambo fulani,na huyo aliyeombwa hakuwa na uwezo wa kutoa hiyo pesa basi akaenda TAKUKURU kuripoti,
Na jamaa wa TAKUKURU wakamwambia asijali wao watampa pesa ampelekee ila ampange siku ya makabidhiano na wao watakuwepo , basi wakapanga siku ya kwenda kumpa pesa alizoomba jamaa...
Siku ilipofika mdaiwa rushwa akapewa pesa za moto kumpelekea mdai rushwa,na wakati wa makabidhiano TAKUKURU walikuwepo wamejificha mahali,
Ile kitendo cha kukabidhiwa tu jamaa akahisi jambo baada ya kuona mazingira hayaelewi ikabidi TAKUKURU watokee hapohapo mwamba akatupa burungutu chini ila ikawa too late alishafikiwa na mkono wa TAKUKURU.......mpaka hivi sasa jamaa yupo ndani....