Othman Kazi alifanya madudu katika urefa akafungiwa maisha, leo anawakosoa waamuzi

Hivi huu utamaduni wa kujadili watu badala ya hoja zào umeletwa na Nani?
Kazi kaweka video za tukio husika Kwa slow motion na mgandisho. Kila Mtu kaona aliyetaka kuona. Wewe badala ya kupinga alichoonyesha unapinga maisha yake ya nyuma. Kwenye Biblia tunaambiwa Paulo alikuwa mnyang'anyi lakini alibadilika kuwa Muinjilisti na akaandika vitabu zaidi ya vitano vinavyoinjilisha mpaka Leo. Kwa hiyo Mkristo amisoma Waraka wa Paulo Kwa Warumi azue hoja kwamba anayekemea dhambi ya dhuluma yeye mwenyewe alikuwa dhulumati?
Chakula kilicho katika sahani chafu sio salama kwa mlaji ,huyu kazi alifaa avalishwe jiwe atumbukizwe pale malagarasi
 
Mimi nikiwa kidato Cha Nne nilichezesha Mpira shule ya Kisarawe na Minaki.

Tangu pale sijawahi kuchezesha Tena Mpira zaidi ya Miaka 10 sasa....

KUCHEZESHA MPIRA SI KAZI NYEPESI.
Urefarii mizinguo sana, kukosea nje nje.
Mimi niliwahi kuchezesha mazoezini tu, tangu siku hiyo sijawahi kulaumu referee hadi kosa liwe very obvious
 
Nchi hii uhuru umepitiliza,yaani mtu aliyeshindwa kusimamia sheria za soka uwanjani na kufungiwa maisha leo hii anawakosoa na kuwafundisha waliopewa dhamana hiyo baada ya yeye kushindwa,

Imenikumbusha serikali yangu aliyefeli ndio anakuwa mwalimu akamfundishe mwanafunzi kufaulu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Alifikiri watu wamesahau!! Kama kuna mtu anajua link ya uzi uliohusika na Kazi kufungiwa atuwekee hapa!!
 
Mimi nikiwa kidato Cha Nne nilichezesha Mpira shule ya Kisarawe na Minaki.

Tangu pale sijawahi kuchezesha Tena Mpira zaidi ya Miaka 10 sasa....

KUCHEZESHA MPIRA SI KAZI NYEPESI.
Kisarawe na Minaki? Kuna sekondari inaitwa kisarawe?
 
Oooh,sio kwamba alikula ila kujitoa akajifanya yeye ni mtoa taarifa ?
Alikula rushwa ...tena tatizo la rushwa ukiila inakuwa kama umechukuliwa akili zako kwa muda na kuanza kufanya maamuzi kutokana na maelekezo ya aliyekupa rushwa....

Na wamempa kichaka cha kupatia ugali wake
 
Referee ni kazi ngumu sana
Ugumu ni pale umeamua kumakosa na kweli umegundua umeshafanya kosa unaona hatari kujikana unaamua ukomae na makosa ya kwanza ili uoneshe msimamo
Kuna wachezaji wanalalamika
Kila tukio kuliona na kuliamua kifasaha ni ngumu
Mimi huwa simlaumu mwamzi
Ni kazi ngumu sitaifanya tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Osman kazi hakufungiwa kwa kuchezesha mpira vibaya au kwa kutokujua sheria za mchezo, bali alifungiwa kwa kwa kupewa fedha na Majimaji; fedha ambazo ni wao walioziripoti na kuzipeleka TFF. Bila wao marefa wenyewe kuiambia TFF kuwa waliletewa fedha na Majimaji, hakungekuwa na ban hiyo.
 
Nchi hii uhuru umepitiliza,yaani mtu aliyeshindwa kusimamia sheria za soka uwanjani na kufungiwa maisha leo hii anawakosoa na kuwafundisha waliopewa dhamana hiyo baada ya yeye kushindwa,

Imenikumbusha serikali yangu aliyefeli ndio anakuwa mwalimu akamfundishe mwanafunzi kufaulu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mrushwa mbaya sana Othman Kazi. Dhulumati na tapeli mkubwa.
 
Nchi hii uhuru umepitiliza,yaani mtu aliyeshindwa kusimamia sheria za soka uwanjani na kufungiwa maisha leo hii anawakosoa na kuwafundisha waliopewa dhamana hiyo baada ya yeye kushindwa,

Imenikumbusha serikali yangu aliyefeli ndio anakuwa mwalimu akamfundishe mwanafunzi kufaulu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kwenye maisha unaweza kukosea , ukajifunza, ukabadilika na hata ukawa funzo kwa wenzio ( Elimu dunia) kisha ukawafunza na wenzio. Sioni ubaya kuwafunza marefa waliopo ili wasije kuwa alivyokuwa yeye.
 
Osman kazi hakufungiwa kwa kuchezesha mpira vibaya au kwa kutokujua sheria za mchezo, bali alifungiwa kwa kwa kupewa fedha na Majimaji; fedha ambazo ni wao walioziripoti na kuzipeleka TFF. Bila wao marefa wenyewe kuiambia TFF kuwa waliletewa fedha na Majimaji, hakungekuwa na ban hiyo.
Sahihi kabisa .TFF walichukizwa Kwa Kazi na wenzake kutoa hiyo taarifa .
 
Osman kazi hakufungiwa kwa kuchezesha mpira vibaya au kwa kutokujua sheria za mchezo, bali alifungiwa kwa kwa kupewa fedha na Majimaji; fedha ambazo ni wao walioziripoti na kuzipeleka TFF. Bila wao marefa wenyewe kuiambia TFF kuwa waliletewa fedha na Majimaji, hakungekuwa na ban hiyo.
Aaaaahhh huu ni uwongo bwanaa....ni uwongo,kwahiyo TAKUKURU hawapo?yaani mtu upewe rushwa then uripoti ktk sehemu husika kisha ufungiwe maisha acha uwongo hapa hakuna mtoto mdogo,unalolisema haliwezekani hata kidogo, nikupe kisa kimoja...

Kuna jamaa aliomba rushwa kwa mtu ili amfanyie jambo fulani,na huyo aliyeombwa hakuwa na uwezo wa kutoa hiyo pesa basi akaenda TAKUKURU kuripoti,
Na jamaa wa TAKUKURU wakamwambia asijali wao watampa pesa ampelekee ila ampange siku ya makabidhiano na wao watakuwepo , basi wakapanga siku ya kwenda kumpa pesa alizoomba jamaa...
Siku ilipofika mdaiwa rushwa akapewa pesa za moto kumpelekea mdai rushwa,na wakati wa makabidhiano TAKUKURU walikuwepo wamejificha mahali,
Ile kitendo cha kukabidhiwa tu jamaa akahisi jambo baada ya kuona mazingira hayaelewi ikabidi TAKUKURU watokee hapohapo mwamba akatupa burungutu chini ila ikawa too late alishafikiwa na mkono wa TAKUKURU.......mpaka hivi sasa jamaa yupo ndani....
 
Badala ya kumjadili mtu kama mtu, ungejadili kwanza kile anachokifanya kama kina tija au la. Nje ya hapo, utakuwa huna tofauti yoyote ile na mpishi maarufu wa chakula kinachoitwa majungu.
Na kibaya zaidi, Majungu Sio Mtaji.
 
Lakini bado unashabikia Simba.
 
Aaaaahhh huu ni uwongo bwanaa....ni uwongo,kwahiyo TAKUKURU hawapo?yaani mtu upewe rushwa then uripoti ktk sehemu husika kisha ufungiwe maisha acha uwongo hapa hakuna mtoto mdogo,unalolisema haliwezekani hata kidogo, nikupe kisa kimoja...

Kuna jamaa aliomba rushwa kwa mtu ili amfanyie jambo fulani,na huyo aliyeombwa hakuwa na uwezo wa kutoa hiyo pesa basi akaenda TAKUKURU kuripoti,
Na jamaa wa TAKUKURU wakamwambia asijali wao watampa pesa ampelekee ila ampange siku ya makabidhiano na wao watakuwepo , basi wakapanga siku ya kwenda kumpa pesa alizoomba jamaa...
Siku ilipofika mdaiwa rushwa akapewa pesa za moto kumpelekea mdai rushwa,na wakati wa makabidhiano TAKUKURU walikuwepo wamejificha mahali,
Ile kitendo cha kukabidhiwa tu jamaa akahisi jambo baada ya kuona mazingira hayaelewi ikabidi TAKUKURU watokee hapohapo mwamba akatupa burungutu chini ila ikawa too late alishafikiwa na mkono wa TAKUKURU.......mpaka hivi sasa jamaa yupo ndani....
Umeandiak lolongo ndefu isiyohusika na Osman Kazi. Kama TAKUKURU ilimkamta kwa kupokea rusha kutoka majimaji, kwa nini hawakumfungulia mashtaka ilihali rushwa yoyote ni kosa la jinai nchi hii.

Kumfungia urefa ilikuwa ni uamuzi wa TFF madai kuwa alipowasilisha ripoti ya mchezo hakuandika lolote kuhusu rushwa hiyo ingawa alikuwa ameshauarifu uongozi kwa mdomo na kuwasilisha fedha kwa uongozi wa TFF. Pesa zile hawakuzipokea bali waliwekewa kwenye mikoba yao, na kupewa fadhila kama kulipiwa hoteli pamoja na yeye kupewa tiketi ya ndege kurudia Dar badala ya kutumia hela ya basi aliyokuwa amepewa na TFF.

Fadhila hizo ndizo zilizoleta wasiwasi na kwa vile alikuwa ameshawasilisha pesa zile TFF ilimtuhumu tu kuwa ali[pokea rushwa kwa vile ripoti yake haikuzungumzia hela hizo pamoja na fadhila zile. Mchezo ulikwisha kwa Majimaji kushinda 1-0 lakini lilikuwa ni bao la halali, wala Mtibwa hawakulalamika kuonewa
 
Chakula kilicho katika sahani chafu sio salama kwa mlaji ,huyu kazi alifaa avalishwe jiwe atumbukizwe pale malagarasi
Ni Kwa sababu mwenye dhambi wa zamani kakosoa dhambi unayoipenda?
 
Umeandiak lolongo ndefu isiyohusika na Osman Kazi. Kama TAKUKURU ilimkamta kwa kupokea rusha kutoka majimaji, kwa nini hawakumfungulia mashtaka ilihali rushwa yoyote ni kosa la jinai nchi hii.

Kumfungia urefa ilikuwa ni uamuzi wa TFF madai kuwa alipowasilisha ripoti ya mchezo hakuandika lolote kuhusu rushwa hiyo ingawa alikuwa ameshauarifu uongozi kwa mdomo na kuwasilisha fedha kwa uongozi wa TFF. Pesa zile hawakuzipokea bali waliwekewa kwenye mikoba yao, na kupewa fadhila kama kulipiwa hoteli pamoja na yeye kupewa tiketi ya ndege kurudia Dar badala ya kutumia hela ya basi aliyokuwa amepewa na TFF.

Fadhila hizo ndizo zilizoleta wasiwasi na kwa vile alikuwa ameshawasilisha pesa zile TFF ilimtuhumu tu kuwa ali[pokea rushwa kwa vile ripoti yake haikuzungumzia hela hizo pamoja na fadhila zile. Mchezo ulikwisha kwa Majimaji kushinda 1-0 lakini lilikuwa ni bao la halali, wala Mtibwa hawakulalamika kuonewa
Hujui lolote kuhusu hili jambo bora ukae kimya tu....

TAKRIMA ni ndugu wa damu wa RUSHWA usijifyatue akili,mazingira inapotumika TAKRIMA ndio itajipambanua....
Sasa hivyo vitu kwanini wasimpe sasa?maelezo yako yanaonesha kutokuwa na uelewa juu ya dhana ya RUSHWA na hekaheka za soka la bongo......
 
Back
Top Bottom