Othman Kazi alifanya madudu katika urefa akafungiwa maisha, leo anawakosoa waamuzi

DullyJr

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
13,983
Reaction score
11,857
Nchi hii uhuru umepitiliza,yaani mtu aliyeshindwa kusimamia sheria za soka uwanjani na kufungiwa maisha leo hii anawakosoa na kuwafundisha waliopewa dhamana hiyo baada ya yeye kushindwa,

Imenikumbusha serikali yangu aliyefeli ndio anakuwa mwalimu akamfundishe mwanafunzi kufaulu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Anatafuta pa kutokea
 
Mimi nikiwa kidato Cha Nne nilichezesha Mpira shule ya Kisarawe na Minaki.

Tangu pale sijawahi kuchezesha Tena Mpira zaidi ya Miaka 10 sasa....

KUCHEZESHA MPIRA SI KAZI NYEPESI.
Nilichezesha mechi ya parokia pale kinesi aaaaah niliapa kitoshika tena filimbi katika maisha yangu....
Kazi ni ngumu mno ile,usipokuwa makini unapigwa ,sikuwahi kumlaumu kipunje wa mbili chali pale ujiji mwananyamala kwanini alikiwa anachezesha mpira akiwa na panga kiunoni....
 
Sheria anazozielezea ziko sawa? Kama ziko sawa na tunaelewa no problem, msikilize sheria anazijua.
 
Badala ya kumjadili mtu kama mtu, ungejadili kwanza kile anachokifanya kama kina tija au la. Nje ya hapo, utakuwa huna tofauti yoyote ile na mpishi maarufu wa chakula kinachoitwa majungu.
Hakina tija katika ustawi wa soka la nchi maana hatuwezi kumtumia mwovu na mvunja sheria na mhaini wa soka letu kama reference ,aache kunyooshea watu vidole wakati yeye ni mchafu tena ananuka rushwa,
Haya maamuzi ya bahasha za khaki yeye ndio alikuwa fundi tena fundi kwelikweli......
Anachokifanya ni kujaribu kuzua taharuki zisizo na tija ili apate huruma ya wadau ili aonekane ana mchango ktk jamii ya soka...

KIFUPI HUYU NI MPUUZI MLA RUSHWA,MAAMUZI YAKE BATILI YAMEWAUMIZA WATU WANA VIDONDA MPAKA LEO.
 
Nimecheza mpira kwa kiwango fulani ,nimekua ktk soka na club fulan hv

Ila katika kitu siwezi ni kuchezesha mpira km refarii
Kwani kuna ugumu gani? Kutafsiri sheria au kutenda haki? Binafsi nishawahi kuchezesha kishule shule na sikupata changamoto labda kwa vile nilikuwa madarasa ya juu.
 
Mie naona nitakua na mahaba ama ya timu au ya mchezaji ,kifupi nitaboronga
 
Nchi hii uhuru umepitiliza,yaani mtu aliyeshindwa kusimamia sheria za soka uwanjani na kufungiwa maisha leo hii anawakosoa na kuwafundisha waliopewa dhamana hiyo baada ya yeye kushindwa,

Imenikumbusha serikali yangu aliyefeli ndio anakuwa mwalimu akamfundishe mwanafunzi kufaulu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hivi huu utamaduni wa kujadili watu badala ya hoja zào umeletwa na Nani?

Kazi kaweka video za tukio husika Kwa slow motion na mgandisho. Kila Mtu kaona aliyetaka kuona. Wewe badala ya kupinga alichoonyesha unapinga maisha yake ya nyuma.

Kwenye Biblia tunaambiwa Paulo alikuwa mnyang'anyi lakini alibadilika kuwa Muinjilisti na akaandika vitabu zaidi ya vitano vinavyoinjilisha mpaka Leo. Kwa hiyo Mkristo amisoma Waraka wa Paulo Kwa Warumi azue hoja kwamba anayekemea dhambi ya dhuluma yeye mwenyewe alikuwa dhulumati?
 
Nchi hii uhuru umepitiliza,yaani mtu aliyeshindwa kusimamia sheria za soka uwanjani na kufungiwa maisha leo hii anawakosoa na kuwafundisha waliopewa dhamana hiyo baada ya yeye kushindwa,

Imenikumbusha serikali yangu aliyefeli ndio anakuwa mwalimu akamfundishe mwanafunzi kufaulu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kukosoa waamuzi mbona kazi rahisi sana
 
Back
Top Bottom