PostGE2025 Othman Masoud: Inakuwaje Rais awe ndiye anaamua kila kitu na kusimamia kila Taasisi?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Makamu wa Kwanza wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, ametoa kauli kali kuhusu mfumo wa utawala na mgawanyo wa madaraka, akisema kuna hatari ya mamlaka muhimu za dola kujikita mikononi mwa mtu mmoja.

OMO JF.png

Akizungumza na Mwandishi wa BBC Sammy Awami Mei 21, 2026, Masoud amehoji namna mfumo ulivyo, akisema: “Inakuwaje leo una Rais ambaye yeye ndio anaamua kila kitu? Ndio anayemchagua Jaji Mkuu, anachagua CAG, anachagua DPP, anachagua sijui nani, halafu yeye ndio anayetoa amri zote ambazo hao wanapaswa waende wakazisimamie... CAG anapaswa akasimamie matumizi, lakini kama aliyeyaidhinisha matumizi pengine ni Rais mwenyewe, CAG anakwenda kukagua vipi?”

Amesema hali hiyo inaweza kudhoofisha uwajibikaji wa taasisi muhimu za serikali, akisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa mgawanyo imara wa madaraka ili kuhakikisha taasisi kama Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zinafanya kazi kwa uhuru na ufanisi zaidi.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, ametoa kauli kali kuhusu mfumo wa utawala na mgawanyo wa madaraka, akisema kuna hatari ya mamlaka muhimu za dola kujikita mikononi mwa mtu mmoja.

Akizungumza na Mwandishi wa BBC Sammy Awami Mei 21, 2026, Masoud amehoji namna mfumo ulivyo, akisema: “Inakuwaje leo una Rais ambaye yeye ndio anaamua kila kitu? Ndio anayemchagua Jaji Mkuu, anachagua CAG, anachagua DPP, anachagua sijui nani, halafu yeye ndio anayetoa amri zote ambazo hao wanapaswa waende wakazisimamie... CAG anapaswa akasimamie matumizi, lakini kama aliyeyaidhinisha matumizi pengine ni Rais mwenyewe, CAG anakwenda kukagua vipi?”

Amesema hali hiyo inaweza kudhoofisha uwajibikaji wa taasisi muhimu za serikali, akisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa mgawanyo imara wa madaraka ili kuhakikisha taasisi kama Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zinafanya kazi kwa uhuru na ufanisi zaidi.

Fvck CCM
Fvck katiba ya mwaka 1977
Fvck muungano
 
Shida ya Tz vyama vipo kupambana dhidi ya vyama vingine, sio chama kipambane kuleta Maendleo
 
Back
Top Bottom