Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Othman ambae pia ndie Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar ameyasema hayo kwa nyakati totauti wakati akiendelea na ziara ya umarishaji wa Chama Mkoa wa kusini Unguja leo April 12 baada ya kukamilika kwa ziara kama hiyo kisiwani Pemba.
Amesema wakati wanatafuta suluhisho la changamoto za kisiasa Zanzibar walikutana na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM ambae ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na kukubaliana kwa pamoja mambo kadhaa ambayo yangekua muarubaini na kumaliza kabisa kilio cha muda mrefu kila ufanyikapo uchaguzi mkuu.
"Cha kushangaza zilipoundwa timu za utekelezaji wa maagizo wenzetu wakageuka kuja na mengine mapya wakati hakua muda wa majadiliano tena.
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa Othman Masoud Othman alipowasili Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja katika mwendelezo wa ziara yake ya ukaguzi wa Chama kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu. Ziara hii ilianzia kisiwani Pemba na inatarajiwa kufikia tamati hapo kesho.