Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Othman Masoud amesema mamlaka makubwa aliyonayo Rais yanaweza kuondoa mfumo wa checks and balances unaohitajika kuhakikisha uwajibikaji. Amesema Rais anateua karibu kila mtu, hali inayofanya maamuzi mengi kutegemea zaidi uamuzi binafsi wa Rais (discretion).
Akizungumzia Tume ya Uchaguzi, Othman amesema kuna tatizo pale Rais anapokuwa na mamlaka ya kuteua watu wanaosimamia uchaguzi, huku yeye mwenyewe akiwa mgombea. Amesema hali hiyo, pamoja na masuala ya Mahakama na namna viongozi wake wanavyoteuliwa, ni miongoni mwa sababu za kuhitajika kuangaliwa upya kwa Katiba, na wamekubaliana kuanza mchakato wa Katiba Mpya.