Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Taarifa ya ACT imeeleza kuwa ziara hiyo imekuja kufuatia mwendelezo wa ziara za visiwa alioanzia Kisiwapanza Mkoa wa Mkoani Pemba.
Mara baada ya kuwasili Kisiwani Tumbatu (Jongowe) viongozi mbalimbali wa Chama na wazee mashuhuri wa kisiwani hicho walifika na kumpokea.
Akiwa eneo hilo la Jongowe alipata nafasi ya kuweka jiwe la msingi tawi la Chama na kuahidi kumalizia uwezekaji wa jengo hilo.
Katika hatua nyengine Othman ambae ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar amesema kuna umuhimu mkubwa wa uimarishaji wa majengo ya Chama kwa kuwa ndio sehemu sahihi ya kufanya shughuli za siasa ambazo zinalenga kudai mabadikiko ya kiongozi.
Awali, Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Omar Ali Shehe amesema ujenzi wa matawi ya Chama na uimarishwaji umekuwa ukifanyika kila mahala na kuwataka wananchi kujitolea kuimarisha Chama chao.