Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
Mgombea urais wa Zanzibar, kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman amesema endapo akiingia madarakani Oktoba 29, 2025, ataanza kusafisha vitendo vya ufisadi vinavyodaiwa kuwepo visiwani humo.
Amesema vitendo vya kifisadi vilivyopo visiwani humo vinasababisha athari mbalimbali ikiwemo wananchi kukosa haki zao, kudhulumiwa ardhi zao, changamoto ambayo amesema imekithiri Pemba na Unguja.
“Siku zote nasema ahadi yangu ni kuirejesha Zanzibar mikononi mwenu, jambo la pili nitasafisha ufisadi uliojengewa mizizi, ili nchi hii iendeshwe kistaarabu.
“Jambo la tatu, nataka nchi isimame katika maadili na silka zake, lakini jingine ni kumwezesha mwananchi, kama kuna uwekezaji basi uwe wa mwanzo kama huna maarifa Serikali itakupa maarifa,” amesema Othman.