Otimbi na timbeli yo: Ukiniheshimu, nitakuheshimu!

Otimbi na timbeli yo: Ukiniheshimu, nitakuheshimu!

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,072
Kazi hufanyi, hutaki kutokwa jasho, umekaa kaa tu bila kujishughulisha halafu unataka watu wakupe pesa, wewe nani?

Wazazi wake hawakujui, kwao hutaki kwenda, mmekutana tu barabarani halafu unalalamika, wewe nani?

Ujinga ni wako. Upuuzi ni wako mwenyewe!

Kazi unaanza kufanya saa nne asubuhi, mchana unajidai umechoka, wakati huo wenzio wanakomaa mpaka jioni. Mshahara ukitoka unataka mlipwe sawa, wewe nani?

Mtaani hawakujui, huongei na watu vizuri halafu unataka utajwe kwenye nyimbo, wewe nani?

Ujinga ni wako. Upuuzi ni wako mwenyewe. Unajitakia mwenyewe!
---

Huu ni wimbo maarufu wa msanii INNOSS unaitwa Yo Pe. Uandishi wa hivi ni mzuri sana. Wimbo unaburudisha na kufundisha.

Tafsiri hiyo siyo rasmi.
 
Stress mbaya sana unaweza jikuta unafagia ofisi yako pasipo kuelewa
 
Back
Top Bottom