Kuna levels tatu za kujitegemea. Level ya kwanza ni kuamini na kujiaminisha kwa binadamu wote ni sawa na kwa umoja wao kama kikundi cha watu wa sehemu fulani wana potentials au talanta za kufikia mafanikio ya kimwili na kiroho. Bila kuamini hivyo unaweka mwanya wa kunyonywa na kutawaliwa na binadamu wengine, au kudumaa.
Hatua ya pili ya kujitegemea ni kuchukuaa hatua zako wewe mwenyewe, kama mtu binafsi au kama kundi la watu kwa spirit ya kujiamini. Imani ni kitu kikubwa sana, na ndio maana ni vigumu kupigana vita vyenye msingi wa imani. Kwa mfano wazungu wanafanya mambo makubwa sana kwa sababu kuna imani fulani inayowasukuma nyuma. Wamarekani wana imani kwamba nchi yao ipo kwa ajili ya kutawala dunia, Wangereza wanafanya vitu vyao kwa sababu ya pride ya kifalme (ndio maana majeshi yao utasikia royal navy, royal air force, charles darwin alifanya utafiti wake kwenye His Majesty Ship Beagle, n.k), Waisraeli walipigana na waarabu lukuki na kuwashinda maana wana imani kwamba wao ni taifa teule, n.k. Sasa sisi Tanzania Nyerere alinuia kujenga taifa fulani lenye misingi ya imani ya utaifa (Nationalistic Zeal), ila akakumbana na kazi ngumu kwelikweli. Kwanza alijikuta anaongoza watu wapumbavu balaa, kila anachotaka kuwaambukiza wanaona kama anawachelewesha kwenye utajiri. Ni upumbavu huo huo aliokumbana nao Nyerere ndio aliokumbana nao Magufuli. Anyway niishie hapo.
Level ya tatu ya kujitegemea ni kufanya mambo yako mwenyewe, yaani kudictate your own fate, kudetermine your own value na kubuild your own things in your own image. Mfano sisi hatuna sababu ya kufahamu Tanzanite inafanya kazi gani ili tuonekane tumejitegemea. Sisi kazi yetu ni kujua kwamba kwa vile Tanzanite ina soko huko nje, basi tutahakikisha tunajitegemea katika kuichimba, kuiongezea thamani na kupata faida zaidi. Kama uwezo huo hatuna kwa sasa tunajijengea huo uwezo, au tutashirikiana na wenye uwezo kwa win-win situation. Yapo mambo yetu tunayoyaona ya thamani na tutayapa thamani kwa vile ni yetu, si lazima tudese kwa wenzetu kujua kama ni ya thamani. Kwa mfano, watanzania tunapenda kula ugali samaki sato, kwa hiyo kwetu sisi hatuhitaji validation ya kwingineko huko kujua kama ugali sato ni chakula cha thamani au vipi. Huo ndio uhuru wa kifikra, uhuru wa kujiamini na uhuru wa kujithamini.