Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Baada ya kutupiwa changa kwa hotuba mbofumbofu iliyofanywa na Muungwana wiki iliyopita, wengi wameona kuwa vita imefika ukingoni na tayari kusalimu amri.
Ukweli ni kuwa tulifanya kosa moja kubwa sana, kufikiri kuwa kuongelea ufisadi tuu, ndio njia pekee kuing'oa CCM au kuleta mabadiliko kwa Watanzania.
KUpigia kelele ufisadi ni sawa na ni wajibu, lakini inabidi tubadilishe mbinu za vita.
Wenzetu kwa hotuba ya Kikwete, maandamano yaliuyofuata na kauli za Kingunge juzi, zinaonyesha wazi kuwa kamwe kelele kuing'oa CCM kwa kutumia ufisadi hakutafanikia. Huko ni sawa na kauli za Upinzani kukimbilia Ikulu bila kujenga chama imara chenye sera zinazoeleweka.
Katika hotuba yake jana kukubali kuwa mgombea wa urais kupitia chama cha Democrat hapa Marekani, Barack Obama alitoa maneno haya, ambayo nayanukuu na kuomba tuyafanye kuwa dira na changamoto ya mapambano mapya ya kuleta mabadiliko nchini Tanzania.
Tumesikia kauli mbovu za viongozi kujitukuza, kuwadharau na kuwapuuza Wananchi wameanzisha vita kati ya Serikali ambayo ni mali yetu na sis wenyewe wananchi.
Inatupasa kubadilisha mbinu z kivita huku tukiendelea kuwapiga makonzi kuhusu ufisadi na uzembe.
Tuanze kuelimisha umma wa Tanzania kuwa wasipumbazwe na changa la macho, kama kweli Serikali ya CCM inafanya kazi kwa manufaa ya Watanzania na si CCM pekee na maswahiba wao mafisadi, basi Serikali ifanye kazi kututumikia na si kutupiga vita!
John Kennedy alitamka wakati alipopokea uraisi
Wikiendi njema!

Our government should work for us, not against us. It should help us, not hurt us. It should ensure opportunity not just for those with the most money and influence, but for every American who's willing to work.
Tumesikia kauli mbovu za viongozi kujitukuza, kuwadharau na kuwapuuza Wananchi wameanzisha vita kati ya Serikali ambayo ni mali yetu na sis wenyewe wananchi.
Inatupasa kubadilisha mbinu z kivita huku tukiendelea kuwapiga makonzi kuhusu ufisadi na uzembe.
Tuanze kuelimisha umma wa Tanzania kuwa wasipumbazwe na changa la macho, kama kweli Serikali ya CCM inafanya kazi kwa manufaa ya Watanzania na si CCM pekee na maswahiba wao mafisadi, basi Serikali ifanye kazi kututumikia na si kutupiga vita!
John Kennedy alitamka wakati alipopokea uraisi
tujiulize swali hili na pia tuiulize CCM na Serikali yake!ask not what your country can do for you - ask what you can do for your country.
Wikiendi njema!