Owen aitabiria Arsenal ubingwa EPL akiitosa Man United top four

Owen aitabiria Arsenal ubingwa EPL akiitosa Man United top four

jjackline

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
111
Reaction score
274
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Michael Owen ametabiri Arsenal kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) msimu ujao wa 2024/2025 huku akishindwa kuiweka Man United katika orodha ya timu nne zitakazomaliza katioka nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Owen ambaye pia amewahi kuichezea Liverpool, anaamini kuwa Arsenal itazima ubabe wa Man City na kutwaa ubingwa wa EPL baada ya kuukosa msimu uliopita ilipozidiwa kwa pointi mbili mwishoni mwa msimu.

Katika utabiri wake alioutoa katika mtandao wa EPL jana, Owen ameiweka Liverpool kumaliza katika nafasi ya pili, Aston Villa kumaliza katika nafasi ya tatu na Man City kumaliza katika nafasi ya nne.

Utabiri wa Michael Owen kuwa Arsenal itachukua ubingwa wa EPL, umefanana na ule wa nyota wa zamani wa Tottenham Hotspur, Darren Bent ambaye naye anaamini kitu kama hicho.
 
arsenal japo ni chama langu ila hata akiwa mbele point 10 na ikawa bado kuna mechi tano msimu uishe bado ntakuwa na wasiwasi
 
Yeah!! Arsenal mwaka huu Wana motisha ya kufanya vzr kuliko city hata Mimi naenda nae
 
Back
Top Bottom