Nimepatwa na mshituko mkubwa...,baada ya kupokea habari za msiba mzito katika sekta ya burudani,mmiliki wa Mzalendo Pub Millenium Towers Ndugu yetu Costa Mowo hatunaye tena..., Costa amefariki ghafla leo katika hospital ya KCMC Moshi kwa kuugua ghafla kwa shinikizo la damu "low pressure" alikuwa mtu wa watu
Nimezipokea habari za kifo cha mshikaji Costa ambaye ni owner wa Mzalendo Pub pale Millenium tower kwa huzuni kubwa. Yaani hata sina la kusema isipokuwa kumshukuru Mungu kwani ndiye mjuzi wa yote..
Mungu amlaze mahala pema peponi - Amin..
Nakumbuka mara ya mwisho naongea na marehemu alikuwa amejiandaa kugombea Ubunge au Udiwani somewhere mkoani Singida. Na kama mjuavyo Mzalendo Pub ndio kwanza ime pick na kuwa lounge ya vijana wa mjini, mara habari hii...
Duh, ama kweli binadamu sii kitu..
Ndio huyu alikua ana onya marafiki zake wa karibu anao wajali baada ya kutembea na wadada wazuri wa mjini ,kuwa yeye kaisha pita kwahiyo wawakalie mbali hao wadada ?