P DIDY wa Maimatha afariki dunia

Mauza uza

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2008
Posts
2,094
Reaction score
1,366
Nimepata habari za kusikitisha kuhusu huyu kijana Parfect Kagisa aka P Didy wa bongo kafariki dunia leo hii.Maisha ndo yalianza kumnyookea lakini Mungu amempenda zaidi.
RIP - Parfect.

source: Globalpublishers.co.tz
 
ukisema wa Maimartha unamaanisha nn kaka, mume/mchumba/rafiki au?
 


Meneja wa Bendi ya Diamond Musica International, Perfect Kagisa aka 'P Diddy wa Maimartha' amefariki dunia mara baada ya kuanguka gafla maeneo ya Mnazi mmoja leo hii.
Hivi sasa mwili wa marehemu uko hospitali ya Muhimbili kwa taaratibu zaidi za kimazishi kwa mujibu wa mtangazaji wa TBC1 TV Benny Kinyaiya.

R.I.P Bro...
 
naskia kadondoka gafla alikuwa anavuka barabara
 
Duh! R.I.P Bro

Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe
 
ukisema wa Maimartha unamaanisha nn kaka, mume/mchumba/rafiki au?

Nyamayao nilikuwa nasoma yale magazeti ambayo sina hakika kama mhariri wake huwa anayapitia Walipenda sana kuandika habari zao kuwa Pdidy alikuwa ni B/F wa Maimartha lakini walishaachana ..
RIP P.DIDI
 
Wadau... Nimepata taarifa za kusikitisha katika tasnia ya burudani kuwa Perfect Kassiga aka P Diddy,aliyekuwa mchumba wa muda mrefu wa mdau burudani na vipodozi nchini Maimartha wa Jesse amefariki ghafla baada ya kuanguka asubuhi hii.... Marehemu P.Diddy ambaye anamiliki share katika bendi ya Diamond Musica,alikuwa akisimamia mazoezi ya bendi hiyo jana jioni kwenye Bar ya Meeda Sinza. Huku akionekana mwenye afya tele.... Pole sana Maimartha... Poleni sana Familia na poleni wadau mbalimbali wa tasnia ya burudani RIP Perfect.
 
Haya magazeti yenyewe ya udaku,hayaaminik.wasijemzulia kijana wa watu.
 
May the Almighty Lord Rest His Soul In Peace, Amen
 
kifo jamni, kweli Mungu aliwek siri kubwa....poleni wafiwa.
 
Poleni sana wafiwa kwa msiba huo mkubwa uliowapata,Mungu amempenda zaidi kuliko nyie,muombeeni.
 
Dah! Poleni wafiwa na ndugu wote kwa kipindi hichi kigumu. May the Almighty Lord Rest his Soul in Eternal Peace, AMEN.
 
Dah pole Mai nipo pamoja nawe katika kipindi hiki kigumu..
 
:confused2: pole sana Mai, Dah Sijui Itakuwaje
 
Mungu aiweke roho ya marehemu pahala pema.
P. K. (rip)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…