Wadau... Nimepata taarifa za kusikitisha katika tasnia ya burudani kuwa Perfect Kassiga aka P Diddy,aliyekuwa mchumba wa muda mrefu wa mdau burudani na vipodozi nchini Maimartha wa Jesse amefariki ghafla baada ya kuanguka asubuhi hii.... Marehemu P.Diddy ambaye anamiliki share katika bendi ya Diamond Musica,alikuwa akisimamia mazoezi ya bendi hiyo jana jioni kwenye Bar ya Meeda Sinza. Huku akionekana mwenye afya tele.... Pole sana Maimartha... Poleni sana Familia na poleni wadau mbalimbali wa tasnia ya burudani RIP Perfect.