Kwanza futa mimate yako na mapovu, P Funk ni mmoja ya watu waliouwa vipaji vya vijana kwa kuwakatalia kurecord kwake, sasa kama yeye alikuwa na Terms zake na Master Jay akawa na terms zake na Mika Mwamba akawa na Terms zake, sasa inakuwaje Terms za Ruge kwenu inakuwa ni tatizo? that's a question.
P Funk hana udhu wa kujifanya ana uchungu na vita hivi dhidi ya ukandamizaji, ninachokiona Ruge ndio mjanja pekee hapa mjini aliyeweza kukamata game ya muziki wa kizazi kipya licha ya kwamba hajui kuimba wala kucheza, he is successful Promota.
Kulikuwa na kina Mike Mhagama hapa enzi za Redio one inaazishwa kulikuwa na kipindi cha Rap na kikafutwa nakumbumbuka nilikutana na Too Proud a.k.a Mr 2 a.ka. Sugu pale BP alipokuwa gate Man alilaani vikali sana kitendo cha Redio one, lakini nashangaa kelele zote siku hizi ni Ruge na Clouds mbona zilikuwepo hizo redio na wameabandon kupromote wasanii?