Inawezekana kesi ya pili producer aliwauzia biti kina mwana FA na AY.
Biti ya nikusaidiaje P. Funk hakumuuzia Profesa Jay.
Ile biti P. Funk aliitengeneza mwenyewe. Siku Profesa Jay kafika studio akamsikilizisha biti na Prof. akaiandikia mistari ya nikusaidiaje then akarekodi.
Na hata Chamilione alivyoirudia biti kwenye Bomboclat, bado ilikuwa mali ya P. Funk.
Kesi ya Tigo AY, Mwana FA na Msando iliendeshwa kwa ujanja mwingi wa Mwana FA, AY na Msando.
Baada ya Mwana FA na AY kugundua Tigo wanatumia nyimbo zao wakaona hapa ni pa kupiga pesa. Wakamtafuta Msando mapema wakamueleza. Msando akawapa ushauri wa kisheria, vitu vya kufanya kabla hawajaanzisha kesi so hapo COSOTA walienda mapema.
Producer si ajabu alizimiwa hapo. Akalipwa hela za zile biti na kina Mwana FA ziwe mali ya Mwana FA na AY bila kujua watu wanakuja kuzifungulia kesi kubwa ya kupiga hela.
Mwana FA ni msomi na ile pesa ya Tigo kaipiga kisomi sana sababu uhalisia wasanii kibao Tigo ilikuwa inatumia call tunes zao kimakosa. Ila wengi masikini wa kutupwa. Mwana FA na AY tu ndio waliopiga bilioni hizo.