P.Funk/Chameleon vs AY/FA/Tigo: Tofauti ikoje hapa?

JAYJAY

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2008
Posts
8,191
Reaction score
8,490
Hizi ni kesi mbili tofauti za kutofuatwa kwa sheria za hakimiliki. Kesi ya P. Funk na Chameleon, producer P. Funk alipigana na kufanikiwa kupata haki yake iliyokaribia kuporwa na Chameleon.

Kwenye kesi ya pili, mbona producer hajahusika hapo. Nini tofauti ya hizi kesi mbili?

Haya wadau msaada hapo.
 
Inawezekana kesi ya pili producer aliwauzia biti kina mwana FA na AY.

Biti ya nikusaidiaje P. Funk hakumuuzia Profesa Jay.

Ile biti P. Funk aliitengeneza mwenyewe. Siku Profesa Jay kafika studio akamsikilizisha biti na Prof. akaiandikia mistari ya nikusaidiaje then akarekodi.

Na hata Chamilione alivyoirudia biti kwenye Bomboclat, bado ilikuwa mali ya P. Funk.

Kesi ya Tigo AY, Mwana FA na Msando iliendeshwa kwa ujanja mwingi wa Mwana FA, AY na Msando.

Baada ya Mwana FA na AY kugundua Tigo wanatumia nyimbo zao wakaona hapa ni pa kupiga pesa. Wakamtafuta Msando mapema wakamueleza. Msando akawapa ushauri wa kisheria, vitu vya kufanya kabla hawajaanzisha kesi so hapo COSOTA walienda mapema.

Producer si ajabu alizimiwa hapo. Akalipwa hela za zile biti na kina Mwana FA ziwe mali ya Mwana FA na AY bila kujua watu wanakuja kuzifungulia kesi kubwa ya kupiga hela.

Mwana FA ni msomi na ile pesa ya Tigo kaipiga kisomi sana sababu uhalisia wasanii kibao Tigo ilikuwa inatumia call tunes zao kimakosa. Ila wengi masikini wa kutupwa. Mwana FA na AY tu ndio waliopiga bilioni hizo.
 
FRESHMAN,

Ahsante kwa kuchangia. Lakini mbona huwa inasemwa kuwa msanii analipia studio time bali creativity bado inaendelea kuwa mali ya producer?
 
JAYJAY,

Hio labla imekuja siku hizi. Maproducer wengi na wasanii wengi Tanzania hawana elimu kubwa. Mwana FA ana masters ya Uingereza. Haikuwa kazi ngumu kwake kumzidi ujanja producer ambae hata Diploma hana.
 
FRESHMAN, Hermy B mbona ni msomi mzuri tu. Tena wa SUA kama sikosei.
 
FRESHMAN,

Kama ni nyimbo zaidi ya moja inawezekana pia zikawa zimefanywa na producers tofauti. Binafsi nilikuwa najua ni wimbo mmoja.
 
Hv walilipwa zote. Tigo si walikata rufaa?
 
Kumbe waliishalipwa?
 
Hela haijifichi.. maisha ay akaoa mnyarwanda, akanunua nyumba marekani na vacation kibao..na mwana fa akaanza trip za kwenda majuu kuangalia mechi tu za manchester utd..

Unafikiri hayo maisha wangeyapata kwa mziki gani.. miaka hii ya WCB
Hv walilipwa zote. Tigo si walikata rufaa?
 
Hawakulipwa hawana hakimiliki ya zile nyimbo walimuuziaga sony kama ilivyo harmonise na nyimbo zake za wcb hana umiliki nazo
 
Ukiona prodyuza hausiki kwenye kesi ya beat ujue walishamalizana na msanii.
Prodyuza alishalipwa chake na beat ni Mali ya MSANII.

mfano laiza wa wcb Yule ameshamalizana na wcb kwa hyo zile beat ni Mali za wcb.
Yeye akishalipwa mshahara wake basi.
 
Sina hakika sana kama walilipwa mpunga mrefu kama ule...

FA na AY ni mabalozi wa Turkish Airlines, ndiyo maana hua unawaona wanapanda ndege hizo hizo tu wakiwa wanaenda mbele,huwezi wakuta wanapanda ndege nyingine tena First Class,.. Kuhusu AY kununua nyumba marekani hiyo ni story tu mkuu wangu. Sio rahisi kama tunavyodhani
Hela haijifichi.. maisha ay akaoa mnyarwanda, akanunua nyumba marekani na vacation kibao..na mwana fa akaanza trip za kwenda majuu kuangalia mechi tu za manchester utd..

Unafikiri hayo maisha wangeyapata kwa mziki gani.. miaka hii ya WCB
 
Hela walilipwa mkuu, hilo la nyumba pia ni kweli. Baada ya kulipwa tu, jamaa ndo wakaoa na AY ndo akanunua nyumba Marekani
 
Tafuta hela za kutosha ila usipige nazo picha.

Nahisi kina AY na FA walishalipwa mabilioni na tigo,FA anapush Range Rover na pia AY kanunua nyumba Mamtoni(USA) ,Mabilioni waliyovuta tigo ni rahisi AY kununua nyumba maana nyumba za kule ukiwa na usd kuanzia laki 350 unapata nyumba nzuri sana even beach front.(Ukitaka kuthibitisha angalia Fine Living House Hunters utaona bei za nyumba).

Tanzania tu nyumba ndio bei ghari sana si umeona Diamond kanunua nyumba ya milioni 400 SA tena prime area lakini kwa bongo tu kiwanja cha 20 kwa 20 kariakoo karibia milioni 800.

Pia FA kaanzisha biashara ya Unyunyu FynByFalsafa.
 
Hela haijifichi.. maisha ay akaoa mnyarwanda, akanunua nyumba marekani na vacation kibao..na mwana fa akaanza trip za kwenda majuu kuangalia mechi tu za manchester utd..

Unafikiri hayo maisha wangeyapata kwa mziki gani.. miaka hii ya WCB
Kwa pesa ile bilioni 1 waliyogawana ndio afanye yote hayo?
 
Kwa pesa ile bilioni 1 waliyogawana ndio afanye yote hayo?

mkuu yaelekea hata ufatilii hiyo kesi, na hujui mahakama iliamuaje, na pesa waliyokuwa wanaidai tigo ni bilion 2 .1 na wala sio bilioni 1
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…