P Square wamfunga mdomo Diamond!

Super Handsome

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2013
Posts
3,844
Reaction score
6,448
Mwanamuziki wa P square, Peter Okoye ameoneshwa kushangazwa na taarifa kwamba mwanamuziki wa bongo fleva Naseeb Abdul alihudhuria harusi yake hivi karibuni nchini Nigeria na kuhudhuriwa na mastaa mbali mbali akiwenmo msukumba gozi wa Totenham Hotspurs Adebayor.

Awali kupitia blogs mbali mbali kulisambaa taarifa kuwa dimond alikua mwanamuziki pekee afrika mashariki aliyealikwa katika sherehe hiyo iliyohudhuriwa na tajiri nambari wani afrika, Aliko Dangote.

Blogs hizo zilikwenda mbali kwa kumpamba diamond kwa vyeo vya ajabu ajabu ikiwemo Michael Jackson wa afrika mashariki jambo ambalo lilisababisha wengi kumponda.

Akihojiwa na kituo cha EATV mara baada ya kuwasili jijini Dar kwa ajili ya shoo iliyopigwa viwanja vya leaders club, Okoye alishangazwa na taarifa za dimond kuhudhuria katika harusi yake.

Okoye alikua akijibu swali aliloulizwaa na mtangazaji wa kipindi cha HotMix Adrian Hilary kuhusu diamond kuhudhuria harusi hiyo ambapo alionesha kushangazwa na jina hilo na kuhoji Diamond ni nani?

Kushangaa huko kulimaanisha licha Diamond kujichezesha mbele ya Okoye siku ya harusi yake lakini mwanamuziki huyo hakua akijua aliyekua akimzungushia viuno vya ngololo ni nani.

Picha ya diamond akikata viuno katika harusi hiyo zimejaa mtandaoni huku zikiwa na maelezo kwamba amealikwa na P-square kwenye harusi hiyo.


Source: Kiu
 
Haaaaaaaaa huyo anapenda kujipaisha.....aibu yake hyo + kisurual chake bas aibu tupu.
 
So ina maana ya kuwa diamond kajificha
 
Mmh inaelekea aliomba lift tu,yaan aalikwe yeye kwa lipi??,yaan mtu akualike halafu asijue uwepo wako wala jina lako?? Too hell
 
Da labda anajua jina la nasibu hajui la diamondo
 
ha! ha! ha! kwa hiyo mr domo alizamia,kweli mzawa wa tandale ni wa tandale tu.
 
Unafanya masihara nn kualikwa na p square??,kwanza amualike kama nani labda??,angekuwa katoka bongo kwenda uko kwa ajili ya hyo harusi apo sawa, ila uko alienda kufanya muzik na davido sijui ndo hayo mambo yakatokea,so it was coincidence unafanya utani nn kualikwa na ma fogo wa africa??,asitake kiki za ajabu na yeye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…