Pablo Franco Kocha Mpya wa Simba SC

Pablo Franco Kocha Mpya wa Simba SC

Tayari kocha kashaanza kulalamika, kasema umri wa wachezaji wengi wa Simba siyo umri wa mashindano.
 
Walisema wanamtaka asie na jina wala CV kubwa aje kuvipatia vyote Simba SC, hii kamari ngoja tuone kama italipa.

Hivi unaweza kuwa na malengo ya kufika mbali kwenye mashindano ya nje na ndani halafu ukamchukua kocha asie na experience ya mashindano husika?

Wanasema wanamtaka asie na jina ili awe na kiu ya mafanikio, kwani mwenye jina ndio anaweza kukubali kuharibu CV yake kizembe kwa kutofikia malengo ya kazi yake?

Hapa naona bora wangetupa sababu nyingine ya kumchukua huyo kocha asiyefahamika, kama ni issue ya mshahara tujue, lakini tusidanganyane na sababu zao walizotoa kwa kumchukua huyo kocha, Simba SC kwa level waliyofiki sio timu ya kuwajaribu makocha, sioni maana ya kumuacha Gomes halafu unaenda kumchukua mwenye CV ndogo zaidi.

#madness.
Watanzania kwa ujuaji hamjambo? Taifa la watu wa porojo na alf ulela! Unaongelea Experience utafikili experience inanunuliwa sokoni kama ndizi!! Au mpira wa Africa ni tofauti na mpira wa Asia, ulaya,na America?! Tofauti yake ni nini? Je kuna kozi maalumu ya kufundisha mpira wa Africa ambayo uyo mwalimu mpya hana? Je hao wenye experience mnaowasema ambao wamekwisha kuja hapa nchini kwa mamia,walifanikiwa kutufikisha wapi?

Mpira duniani ni uleule na mpira una njia zake na mifumo yake ya kupitia ili uwe bora, kuanzia ngazi ya mchezaji tangu akiwa mtoto,na pia mifumo ya utendaji kiuongozi, ambalo ndio tatizo africa tunapungukiwa nalo, kupata wachezaji ambao hawana misingi ya kimchezo na kuwa na viongozi wasiojua mifumo ya kiuongozi ikichangiwa na umaskini na ujinga wa watu wetu ndio maana hatufanikiwi.
Sio suala la makocha,kusema kocha hana experience ni ushabiki maandazi na kuficha matatizo yetu.
 
Back
Top Bottom