Pacha wajinyonga hadi kufariki baada ya kukorofisha na mama yao Pemba

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2009
Posts
19,009
Reaction score
22,509
Watoto wawili wa kike, ambao ni mapacha wenye umri wa miaka 11 na wanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Kizimbani, wamekutwa wakiwa wamefariki baada ya kujinyonga. Tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Kwale Mpona, Shehia ya Finya, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Akizungumza na Swahili Times, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, (SACP) William Mwampaghale amesema tukio hilo limetokea Novemba 17, 2025 majira ya saa 4:30 asubuhi, ambapo uchunguzi wa awali umebaini kuwa watoto hao waliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kukorofishana na mama yao kuhusu kufanya kazi za nyumbani.

“Waligoma wakaondoka nyumbani, kwa hiyo mama yao baadaye akaanza kuwatafuta, ndipo akakuta miili hiyo imening’inia kama mita 100 kutoka kwenye nyumba yao.

Sisi kama Jeshi la Polisi tunaendelea kuchunguza zaidi tujue kama kweli ni ugomvi tu huo ama kuna sababu nyingine iliyopelekea watoto hao kujinyonga,” ameeleza Kamanda.

Aidha, amesema miili hiyo imekabidhiwa kwa wanafamilia kwa ajili ya taratibu za mazishi.
------------------
"NAJARIBU KUWAZA WALIWEZAJE KUSHAURIANA KUJINYONGA NA WAKAKUBALIANA"

-–----------------

Chanzo: Swahilitimes.
 
Miaka 11..🤔🤔
 
Hao bila shaka walikuwa pacha wa kufanana "identical twins" maamuzi na nafsi zao hazipishani.
Sisi kama binaadam hatuwezi kubadili chochote maana ishatokea.
Watoto mwendo wameumaliza...
Tuwaache walale salama!
 
Watoto wawili wa kike, ambao ni mapacha wenye umri wa miaka 11 na wanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Kizimbani, wamekutwa wakiwa wamefariki baada ya kujinyonga. Tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Kwale Mpona, Shehia ya Finya, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Akizungumza na Swahili Times, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, (SACP) William Mwampaghale amesema tukio hilo limetokea Novemba 17, 2025 majira ya saa 4:30 asubuhi, ambapo uchunguzi wa awali umebaini kuwa watoto hao waliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kukorofishana na mama yao kuhusu kufanya kazi za nyumbani.

“Waligoma wakaondoka nyumbani, kwa hiyo mama yao baadaye akaanza kuwatafuta, ndipo akakuta miili hiyo imening’inia kama mita 100 kutoka kwenye nyumba yao.

Sisi kama Jeshi la Polisi tunaendelea kuchunguza zaidi tujue kama kweli ni ugomvi tu huo ama kuna sababu nyingine iliyopelekea watoto hao kujinyonga,” ameeleza Kamanda.

Aidha, amesema miili hiyo imekabidhiwa kwa wanafamilia kwa ajili ya taratibu za mazishi.
------------------
"NAJARIBU KUWAZA WALIWEZAJE KUSHAURIANA KUJINYONGA NA WAKAKUBALIANA"

-–----------------

Chanzo: Swahilitimes.
Ni mapacha, kukubaliana kufanya lao ni rahisi sana! Watoto wapewe mapenzi ya dhati, sio kuwafanya vijakazi. Akina Mama awe kama Samia, shurti watoto wajitoe roho
 
Back
Top Bottom