Ndabiti Emmanuel Njonde
New Member
- Jun 9, 2023
- 3
- 3
Pachua ni kitendo Cha kutegua ficho kwa kuweka wazi, kionekane kile kilichomo ndani. Hivyo basi, mimi leo napachua kile kilichomo katika malezi kama shule ya kwanza ya ukuzaji na uleaji.
Malezi ni shughuli nzima ya utunzaji kwa lengo la kukuza kuanzia hali ya chini mpaka juu pale ulipokusudia kumfikisha na kuamini kuwa atakuwa salama atakapofikia hatua ya kujitegemea.
Katika jamii kumekuwa na malezi tofauti tofauti na hii imesababisha jamii kuharibika na kuendelea kuaribika kwa kushambulia kizazi kipya kwa nguvu na kwa haraka.
Ninapo zungumzia kuharibika, kuna mahali kwenye malezi Kuna udhaifu. Na huu udhaifu umepelekea kuharibika kwa misingi ya malezi.
Kuna aina mbili za malezi, ni ile ya kujilea kama vile unavyotaka kuwa na ya pili ni ile unavyotaka awe. Hapa mimi nitaelezea kwa ufupi kidogo, kwani malezi hayana mwisho, tunapojilea katika maadili mema bila kuvunja yale mema, ndivyo tutakavyo weza kulea wengine katika maadili hayo mema. Nukuu ya wahenga husema, "mtoto umleavyo, ndivyo akuavyo," na mimi najazia kwa kusema, "kizazi huharibiwa na wazazi"
Kumekuwa na sintofahamu katika jamii, mathalani fulani ni kijana mwema, na mwengine si kijana mwenye maadili (mema) na wakati mwingine yule mwenye maadili (mema) anavunja maadili aliyo nayo, naye anakuja kufanana na yule aliye na maadili ya ovyo. Hii yote husababishwa na misingi ya malezi.
Kwangu mini kuna msingi mmoja mkuu katika malezi, mbali na gharama za malezi kwa kumpa kumpa mtoto elimu, kumjali kiafya na kumpa malazi. Mbali na hayo kwangu hupendelea mtoto kumjulisha thamani yake kwa kumpa picha za kufikirika zenye kumwonyesha hapo baadae atakavyo kuja kuwa bora kwa thamani. Pia namuongezea jambo la uwajibikaji.
Narudi kidogo kwenye maisha, Kuna msemo wanasema kwenye jamii zetu asiye jua maana yake, hana maana. Nataka tuone maisha ni nini kwanza. Maisha kwangu ni kuenenda katika furaha, upendo na kuwajibika katika mazingira sahii na wakati sahihi.
Sasa kama tutaenenda katika furaha, upendo, na kuwajibika katika mazingira sahihi, kama kazini, katika biashara na katika jamii, hata yule anayelelewa ataishi katika misingi hiyo, japo hivi sasa hali hii ya maisha katika familia nyingi haipo.
Utakuta baba na mama hawaishi katika hii ali ya maisha bora, je, yule anaye lelewa atakuwa anajifunza nini kupitia macho yake juu ya wale wanaomlea. ? Ndiyo narudi pale niliposema Wazazi huharibu kizazi
Baba na mama ni wazazi na ni viongozi. Hapa nagusia hata kwa wale walio katika majukumu ila bado hawajaoa au kuolewa, walio na watoto na wasio na watoto, na wenye kutarajia kufikia ngazi ya ulezi hapo baadae.
Kiongozi kwangu ni yeyote mwenye kutimiza majukumu. Kwa nini nagusia uongozi ? kwa sababu popote pale panapo hitajika malezi, lazima viongozi wapepo, na kwa bahati nzuri malezi hayaanzii katika jamii inayo kuzunguka tu, bali huaanzia ndani katika familia.
Tukumbuke pia kwamba familia ndiyo serikari ya kwanza duniani. Yenye viongozi ambao ni wawili baba na mama, na hawa ndio walezi wakuu ndani ya familia na hata nje ya familia.
Laiti walezi wangejua nafasi yao ya uongozi, wangejua kulea.
Kwanza kiongozi ni nini na kuna nini katika neno lenyewe "KIONGOZI"?
KIONGOZI
K- kujilea na kulea katika maadili mema, na kukubali kushaurika na kushauri ( mke na Mume);
I- ielewe tabia ya watu unao watawala (watoto);
O- onyesha uwajibikaji kwa vitendo;
N- Nena kauli thabiti (kwa kiongozi mwenzako na kwa wale mnaowalea, haijalishi kama ni ndani ya familia au nje)
G- gawa madalaka kwa unaowalea, ( maana yake ni kwamba wafunze kuwajibika kwa kuwaajibisha)
O- ondoa uonevu,( uonevu upo, unapo lea ukiondoa uonevu maana yake umeondoa unyonge ambao baadae ungeleta madhara kama chuki zilizokithiri)
Z- zuia migogoro kwa unaowalea, au unaowatawala( ninamaanisha ni Ile furaha na upendo ili ipate kudumu katika maana Ile ya maisha niliyoitoa.
I- inua maisha ya watu unowatawala ( nagusia kuwapa elimu, malazi, kujali afya, chakula na kumwonyesha thamani yake juu ya msingi bora wa maisha)
*Hivyo basi, walezi ni viongozi.
Sasa, kama walezi hawajui kanuni za uongozi, je kitakacholelewa kitakuwa bora ? Je, kikikua nacho kitaweza kulea wengine ?Kuna mahali nilisema wazazi ndio wanaoharibu kizazi, hivyo basi walioharibika wakichangamana na walio wazima, kile kizima nacho kitaharibika na kuoza.
Katika malezi, kuna changamoto ya wazazi na ya watoto. Hapa Kuna madarasa mawili tofauti, watoto wanapokuwa kwenye michezo yao wanafundishana wenyewe, na hii ni ngumu sana mzazi kujua nini mwanae amejifunza kutoka kwa wenzie, na kuna ushawishi mkubwa sana wanapokutana watoto kwa watoto.
Kwa hivi sasa, dunia ipo katika kiganja cha utandawazi. Huu utandawazi umefanya dunia kuwa kijiji, ila pia imeongeza mmomonyoko wa maadili katika malezi, kiasi kwamba malezi yamekuwa ni jambo gumu.
Kumekuwa na mchezo wa jenga bomoa, wazazi wanaweza wakawajibika katika malezi mazuri, ila utandawazi ukabomoa kupitia katika ushawishi wa rika.
Na hapa ndipo kwenye changamoto kubwa ya kimaleze kwa watoto, kutokana na uhuru wa kimtandao usio na mipaka, na imepelekea kuathiri hadi walezi pia.
Pia kuna njia rafiki zaidi ya kuboresha malezi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa walezi na walelewaji. Elimu za malezi ziwekwe kwenye mafungu mawili, fungu la kwanza liwe la walezi, wafundishwe na wakumbushe majukumu yao wakiwa kama walezi, na elimu nyingine itolewe kwa watoto wakiwa shuleni ambapo wafundishwe ni jinsi gani wanaweza kubakia salama dhidi ya mashambulio ya utandawazi, na pia kutetea yale mema waliyo jifunza, na baki kama mwongozo wa maisha yenye maadili mema.
Jamii sasa yapaswa kuwa na msimamo mmoja wa malezi, maana umoja ni nguvu. Huu umoja utaweza kuleta mabadiliko chanya haraka zaidi, kuliko familia moja moja ikipambana.
Na ili msimamo wa malezi uwekwe na ufuatwe, je, viongozi wa kwenye jamii wanafahamu hii changamoto iliyopo kwenye malezi ?
Ni wajibu wetu kuwakumbusha, huku nasi tukiendelea kuwa walezi bora kwa kizazi chetu na kizazi kingine, ili kuweza kujenga taifa lenye watu werevu na tusipofanya hivyo, jua litafunikwa na kiza.

Upvote
2