Leo ametangazwa tu, uteuzi umefanywa na papa kitambo huko, kanisa Lina sheria kali sana zinazoongoza michakato hii na jambo kuu linalotawala ni usiri mkubwa, kuanzia mapendekezo, machaguo (options), kuteuliwa, kutangazwa na kuwekwa wakfu, mfano ulio wazi: kati ya kutangazwa (mfano, askofu Bududu kutangazwa leo tarehe 26 Feb mpk kuwekwa wakfu - maaskofu wasaidizi hawasimikwi, sheria inatoa muda wa miezi 3) so, what if kama kati ya kuteuliwa na kutangazwa napo pia ni miezi mitatu? Ikiwa ni hivyo (mfano) Ina maana askofu mteule ameteuliwa mwaka jana mwishoni, kipindi kile Mzee alikua na Afya yake kamili gado anasafiri toka nchi hii kwenda Ile, bara hili na lile na kufungua malango ya makanisa makuu kuashiria jubilee ya miaka 2025 ya ukatoliki duniani.... Hongera askofu Bududu (PhD Christian spirituality), Hongereni nyuki wa Tabora.