PostGE2025 Padre Kitima akumbusha: Tulionya, taifa linaelekea pabaya

PostGE2025 Padre Kitima akumbusha: Tulionya, taifa linaelekea pabaya

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
"Tulisema haya yasipozingatiwa nchi haitakaa salama tunaelekea pabaya. Tuliongea taifa linaelekea pabaya tulishaona, lakini kupuuza viongozi wa dini ni hatari sana kwa sababu viongozi wa dini hawana maslahi binafsi kwenye taarifa zinazohusu uhai wa mtu.​
​
Kwahiyo kusema watu wamenunuliwa si kweli, kuna matatizo yanayoendelea ya msingi ya nchi ambayo hayajashughulikiwa, watu wanatekwa, wanapotezwa, wanauawa."​

Padre Charles Kitima, Katibu mkuu wa baraza la maaskofu katoliki Tanzania akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 01, 2025.

 
Hivi familia ya Mzee Kibao, Sativa, Mdude, Soka, Polepole .

Wanahitaji malipo kuingia barabarani kwenye maandamano kuonyesha hisia zao kwa yanayowagusa?

Hapo tunaongelea ni watu wenye kaka, dada , mjomba , shangazi , binamu, rafiki, mfanyakazi mwenza , mke , mtoto , wajukuu.

Mbegu ilipandwa muda mrefu sasa ni mavuno .

Itaanza upepo wa maandamano halafu ghafla itaanza visasi kwa kuviziana ili maumivu yaende upande wa pili.

Haiingi akilini polisi wanavamia kwa mtu wanajitambulisha ni polisi wakiwa hawana sare wanampiga na kuondoka na mtu halafu familia inaenda polisi hawajui wanaenda mahakamani napo hawajui mtu alipo.

Mnafikiri hizi familia zikikosa haki katika vyombo rasmi zitachukua hatua gani zaidi ya kutafuta haki[kisasi] katika mfumo wanaoo unafaa?

Mfano huyu mjukuu wa Mzee Kibao pichani kwa sasa hana babu tena wa kutaniana na kucheza nae kwa sasa atafichwa.

Akikua anaambiwa babu yako alishushwa kwenye gari mchana kweupe akaenda kutobolewa macho na hatimaye kumwagiwa tindikali kisha akatelekezwa ununio halafu rais wa kipindi hicho akasema KIFO NI KIFO.

Mmeona jinsi gani waasi/magaidi wanavyotengenezwa?

Je huyu mtoto nae akianza kumsaka mjukuu wa Samia miaka hiyo 2060 ukute serikali ikiwa chama kingine , katiba nyingine, watu wengine ili alipe kisasi kuna mtu anaweza kumbadilisha japo maneno aliongea bibi mtu na sio mjukuu??
images (15).jpeg
 
Back
Top Bottom