PostGE2025 Padre Wigira: Tusisahau waliouawa katika matukio ya uchaguzi wa 2025

PostGE2025 Padre Wigira: Tusisahau waliouawa katika matukio ya uchaguzi wa 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
52,815
Reaction score
103,955

Msimamizi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padre Dennis Wigira, amesisitiza umuhimu wa kuwakumbuka na kuwaombea watu waliopoteza maisha kwa kuuawa katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, akieleza kuwa tendo hilo ni sehemu ya kawaida ya imani na ufuasi wa Kikristo.

Akihubiri katika Misa Takatifu ya kuwaombea marehemu hao, Padre Wigira amesema baadhi ya watu wasioufahamu vizuri msimamo wa Kanisa Katoliki wanaweza kulitafsiri tofauti tendo hilo, lakini kwa waamini, kuwakumbuka waliopoteza maisha kwa imani na katika mazingira mbalimbali ni sehemu ya ushuhuda wa Kikristo.

Akitolea mfano mashahidi wa Uganda, Padre Wigira ameeleza kuwa Kanisa linaendelea kuwakumbuka waliotoa maisha yao kwa ajili ya imani, si kwa lengo la kuchokonoa mambo ya kale, bali kutambua thamani ya ushuhuda wao. Amesisitiza kuwa kumbukumbu ya mashahidi na watu waliopoteza maisha kwa kuuawa inapaswa kusaidia jamii kutafakari kwa kina kuhusu thamani ya uhai wa binadamu na wajibu wa kulinda utu wa kila mmoja.

Padre Wigira ameonya kuwa kusahau matukio kama hayo na kuendelea na shughuli za kila siku bila kutafakari maana yake kunaweza kudhoofisha utambuzi wa thamani ya maisha ya binadamu, na hivyo kuchangia kuendelea kwa chuki, migogoro na mauaji.

Wito wake ni kwa jamii kuendeleza kumbukumbu yenye kujenga, inayohamasisha upendo, amani, mshikamano na heshima kwa uhai wa kila binadamu.
.
.
www.tec.or.tz
#KanisaKatolikiTzTEC
 
Back
Top Bottom