upupu255
Senior Member
- Sep 4, 2024
- 119
- 144
Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar, Anselmo Mwang’amba amefariki dunia Februari 27, 2025 kisiwani Zanzibar.
Taarifa iliyotolewa na Askofu wa jimbo hilo, Agustino Shao imesema mipango ya mazishi inaendelea.
“Roho ya padri Anselmo Mwanga’mba ipate rehema kwa Mungu ipumzike kwa amani,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Akizungumza na Mwananchi Digital leo Februari 28, 2025, Katibu Mkuu wa Jimbo hilo, Padri Cosmas Shayo amesema wapo kwenye vikao vya mazishi.
Itakumbukwa mwaka Septemba 2013, Padri Mwang’amba alimwagiwa tindikali na kulazwa katika Hospitali ya Mnazimmoja kisha kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Tukio hilo lilitokea katika Mtaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi na kujeruhiwa usoni, kifuani na mkononi.