Padri Kitima aadhimisha misa ya shukrani baada ya kutoka hospitali, asema 'Mungu hatakaa kimya, atajibu sala zetu'

Ni bora mwanasiasa akafanya dini kuliko kiongozi wa dini kufanya siasa
 
Attachments

  • Screenshot_20250601_171956_Samsung Internet.jpg
    Screenshot_20250601_171956_Samsung Internet.jpg
    294.4 KB · Views: 24
Unajua madhara ya hicho unachiandika mkuu!!
Mi sio shabiki wa Dini lakini sio vizuri kuandika jambo ambalo huna ushahidi nalo!!
 
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padri Dkt. Charles Kitima ameongoza Adhimisho la Misa Takatifu ya shukrani kwa mara ya kwanza baada ya kutoka hospitali alikokuwa anapatiwa matibabu kwa takribani mwezi mmoja baada ya tukio la shambulizi dhidi yake.

Padri Kitima ameongoza adhimisho hilo katika Kanisa la Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili lililopo TEC-Kurasini, Dar es salaam leo Juni 3, 2024 pamoja na mapadri, watawa na wafanyakazi wengine wa Sekretarieti ya TEC, kwa nia ya kumshukuru Mungu kwa kumponya.

Akitoa homilia katika adhimisho hilo Padri Kitima amemshukuru Mungu kwa kumponya dhidi ya shambulizi lililolenga kukatisha uhai wake, huku pia akiwashukuru watu wote kwa sala na matashi mema katika kipindi chote cha matibabu yake.

“Tunamshukuru Mungu kwa wema wake, pia tunawashukuru watu wote walioguswa na tukio lile. Tuombe ili Kanisa lizidi kuwa imara siku zote bila kutetereka. Tukumbuke kuwa Kanisa Katoliki ni taasisi inayotegemewa na watu wengi, ni sauti ya watu wasio na sauti, ni msindikizaji wa wanyonge. Tuliombee Kanisa letu lizidi kuwa mwanga na matumaini ya Watanzania” ameeleza Padri Kitima.
Aidha Padri Kitima amewataka wana Sekreatarieti ya TEC kuyapokea mambo yote yaliyotokea kwa jicho na moyo wa imani akisisitiza kuwa katika mambo yote ambayo Kanisa linayasimamia kwa ajili ya wanyonge, Mungu atayasikiliza.

“Mungu hatakaa kimya, atajibu sala zetu. Tuwe imara katika kazi zetu, tukumbuke kuwa hata mitume walipata misukosuko. Tusirudi nyuma, tubaki katika imani thabiti” ameongeza.
 
MkMungu ni mwema,kupona kwako ni anguko la mzanzibar,naomba tuendelee tulipo ishia
 
Hahaha, Polisi Walituambia ni mlevi, vipi katoka sober house?

Polisi walisema wanasubiri atoke sober house wamuhoji ili lukamilusha upelelezi, wamesha muhoji au bado?
 
Hii ndio Taarifa mpya aliyoitoa yeye mwenyewe kama alivyonukuliwa na Azam TV.

Screenshot_2025-06-03-14-19-57-1.png
Screenshot_2025-06-03-14-20-09-1.png

Wakati hayo yakiwa hivi, Juzi Kamanda Murilo aliwaeleza Waandishi wa Habari kwamba Uchunguzi wa sakata hilo ungali unasubiri Maelezo ya Kitima.

Swali letu ni hili, Je kama Dkt Kitima angeuawa maelezo hayo wangeyatoa wapi au ndio ingekuwa yale yale ya Kosa la Marehemu ........?
 
Hii ndio Taarifa mpya aliyoitoa yeye mwenyewe kama alivyohojiwa na Azam TV.

View attachment 3354629View attachment 3354633

Wakati hayo yakiwa hivi, Juzi Kamanda Murilo aliwaeleza Waandishi wa Habari kwamba Uchunguzi wa sakata hilo ungali unasubiri Maelezo ya Kitima.

Je kama angeuawa maelezo hayo wangeyatoa wapi au ndio ingekuwa yale yale ya Kosa la Marehemu ........?

Huo ndio Ukweli wenyewe.

Lengo kuu kabisa la shambulizi dhidi ya Padre Dkt. Kitima lilikuwa ni kumuua, na wala siyo vinginevyo.
It was an Assassination Plot against the Cleric, a failed Assassination Plot.

That Assassination Plot was well planned, but it failed at the stage of execution. Shetani alisimama upande wa Wauaji, na Mungu alisimama upande wa Padre Dkt. Kitima.
 
Sitakufa Bali nitaishi milele

kufa mwili sio kufa roho

Unaweza kuniua ukanisaga na kunichoma hata majivu yangu yasionekane

Lakini amini yakwamba Mimi ninaisha na nitaishi !!!
 
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padri Dkt. Charles Kitima ameongoza Adhimisho la Misa Takatifu ya shukrani kwa mara ya kwanza baada ya kutoka hospitali alikokuwa anapatiwa matibabu kwa takribani mwezi mmoja baada ya tukio la shambulizi dhidi yake.

Padri Kitima ameongoza adhimisho hilo katika Kanisa la Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili lililopo TEC-Kurasini, Dar es salaam leo Juni 3, 2025 pamoja na mapadri, watawa na wafanyakazi wengine wa Sekretarieti ya TEC, kwa nia ya kumshukuru Mungu kwa kumponya.

Akitoa homilia katika adhimisho hilo Padri Kitima amemshukuru Mungu kwa kumponya dhidi ya shambulizi lililolenga kukatisha uhai wake, huku pia akiwashukuru watu wote kwa sala na matashi mema katika kipindi chote cha matibabu yake.

“Tunamshukuru Mungu kwa wema wake, pia tunawashukuru watu wote walioguswa na tukio lile. Tuombe ili Kanisa lizidi kuwa imara siku zote bila kutetereka. Tukumbuke kuwa Kanisa Katoliki ni taasisi inayotegemewa na watu wengi, ni sauti ya watu wasio na sauti, ni msindikizaji wa wanyonge. Tuliombee Kanisa letu lizidi kuwa mwanga na matumaini ya Watanzania” ameeleza Padri Kitima.

Aidha Padri Kitima amewataka wana Sekreatarieti ya TEC kuyapokea mambo yote yaliyotokea kwa jicho na moyo wa imani akisisitiza kuwa katika mambo yote ambayo Kanisa linayasimamia kwa ajili ya wanyonge, Mungu atayasikiliza.

“Mungu hatakaa kimya, atajibu sala zetu. Tuwe imara katika kazi zetu, tukumbuke kuwa hata mitume walipata misukosuko. Tusirudi nyuma, tubaki katika imani thabiti” ameongeza.
View attachment 3354311View attachment 3354314
Sasa si amshukuru Mungu kulialia kunasaidia nini, km anamfahamu ampeleke mahakamani ila atulize bakuli atapotezwa kweli na maisha yakaendelea km kawa
 
Vita bado mbichi
 
Back
Top Bottom