ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
My Take: Hii Kauli inatuma ujumbe Fulani ,wajuzi watujuze.
Moja ya tukio lililovuta hisia za washiriki wa kilele cha Kongamano la tano la Ekaristi Takatifu la Kanisa Katoliki ni hili la wanasiasa wa CCM na Chadema kuwa pamoja.
Kilele hicho kimefanyika leo Jumapili, Septemba 15, 2024 katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Maaskofu zaidi ya 20, Mapadri, watawa wa kiume na kike wameshiriki. Mgeni maalumu akiwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko.
Utambulisho uliofanywa na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima uliibua shangwe na furaha. Ni baada ya kuwaita madhabahuni, makatibu wakuu, Dk Emmanuel Nchimbi (CCM), John Mnyika (Chadema) na Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara, Tundu Lissu.
Dk Nchimbi, Lissu walikuwa wamekaa eneo moja, kuna wakati walionekana wakizungumza.
Waliposimama, Dk Nchimbi na Mnyika waliokuwa mbalimbali, walisogeleana, wakasalimiana na kisha wakakumbatiana kwa tabasamu kisha wakaenda kupanda madhabahuni.
Wakati wakipanda madhabahuni, Padri Kitima akawaeleza Mnyika na Dk Nchimbi: "Msaidieni ndugu yenu Tundu Lissu, demokrasia ina gharama zake, tumesema udugu kuponya ulimwengu nyinyi nyote ni ndugu si mnaona nguvu ya ekaristi."
Msingi wa kauli hiyo ya Padri Kitima akiwataka Mnyika na Dk Nchimbi kumsaidia Lissu ni kutokana na majeraha aliyoyapata Septemba 7, 2017 baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na 16 zikimpata mwilini, hivyo kusababisha atembee kwa tabu na kupata shida kupanda ngazi za madhabahu.
Soma Pia: Dkt. Emmanuel Nchimbi, Mnyika na Tundu Lissu wapandishwa madhabahuni na Padri Dkt. Charles Kitima