GE2025 Padri Kitima: Muda bado upo, wakae Mezani kujadili dosari za Uchaguzi – Kwanini waenguliwe wale wale tu?

GE2025 Padri Kitima: Muda bado upo, wakae Mezani kujadili dosari za Uchaguzi – Kwanini waenguliwe wale wale tu?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima amesema, "Muda hajapita wa kukaa mezani sasa hivi kuna Miezi Mitatu [Julai kuna Agosti na Septemba], Watu hawawezi kushindwa kukaa Mezani, wakae Mezani wajadiliane hizi dosari ambazo watu zimewakera wengi, tuziondoe, kusema hatutapeleka Kura Feki kwenye Kituo, hatutaengua Mtu kwa kumuonea"

"Nashangaa wanaoenguliwa ni Vyama hivi tu lakini Chama Kimoja hakuna anayeenguliwa hata mmoja, hakuna anayekosea kuandika jina"

 
Apewe ujumbe wa kamati kuu Chadema, analichafua kanisa. Kanisa limekubali kutumika kisiasa. Huu ni udhaifu wa kitaasisi.

Kitima ameshindwa kuficha maslahi binafsi aliyonayo kwa msingida mwenzie Lissu. Kanisa Katoliki kuendelea kumuacha Kitima kuwa kiongozi wa Kanisa ni udhaifu wa kimfumo dhidi ya kiongozi.

Kwamba Kanisa Katoliki lipo tayari kumlinda kiongozi anayepigania maslahi binafsi kwa kujikinga kwenye ngao ya dini.
 
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Dkt. Charles Kitima, amewashauri viongozi wa kisiasa nchini, serikali na wadau wote wa uchaguzi kukaa mezani haraka iwezekanavyo ili kujadiliana na kuondoa dosari zilizozua sintofahamu kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.Akizungumza katika mahojiano maalumu na Jambo TV, Padri Kitima amesema bado kuna muda wa kutosha kwa pande husika kuzungumza kwa nia njema ili kuhakikisha Watanzania wanashiriki uchaguzi huru, wa haki na wenye kuaminika.

"Watu wakae mezani, yanayoweza kufanyika sasa yafanyike. Hii ni Julai, bado kuna Agosti na Septemba. Muda haujaisha. Dosari hizi zimewakera wengi, tuziondoe," amesema Padri Kitima.Ameeleza kuwa, badala ya kutaka kususia uchaguzi, viongozi wa vyama vya siasa waamini kuwa serikali inaweza kutoa ahadi ya kweli na yenye dhamira ya kuondoa vitendo vya udhalimu na kutozingatia sheria katika mchakato wa uchaguzi.

“Wanaotaka kususia uchaguzi waamini kwamba ahadi itakayotolewa na serikali kwamba hizi dosari hazitakuwepo, waamini kweli dosari hizo hazitakuwepo, na wakishaamini washiriki, halafu siku ya uchaguzi watakapoona zimekiukwa basi watakuwa na fursa ya kuthibitisha kwamba basi kwa mantiki hii labda twende mahakamani, au kwa mantiki hii hayo mabadiliko yafanye kwa lazima kupitia serikali mpya itakayokuwa imeingia, lakini kusema kwamba lazima tukae tubadilishe sheria zote na nini ndani ya muda uliobaki au tuahirishe uchaguzi binafsi ninaona kule tunaenda mbali mno, hebu turudishe kwanza uadilifu, na kuondoa dosari hizi", ameeleza.

 
Mlikua mtikisa kiberiti eeeh! tukutane 2030.
1000073785.jpg
 
Apewe ujumbe wa kamati kuu Chadema, analichafua kanisa. Kanisa limekubali kutumika kisiasa. Huu ni udhaifu wa kitaasisi.

Kitima ameshindwa kuficha maslahi binafsi aliyonayo kwa msingida mwenzie Lissu. Kanisa Katoliki kuendelea kumuacha Kitima kuwa kiongozi wa Kanisa ni udhaifu wa kimfumo dhidi ya kiongozi.

Kwamba Kanisa Katoliki lipo tayari kumlinda kiongozi anayepigania maslahi binafsi kwa kujikinga kwenye ngao ya dini.

Crap from empty brain.
 
Hivi CCM huwa hamuonagi AIBU??..chama hakina WAZEE kabisa???..hakika INASHANGAZA
 
Anamwambia nani?huyu mzee hajajifunza tu kutenganisha siasa na dini?
 
Apewe ujumbe wa kamati kuu Chadema, analichafua kanisa. Kanisa limekubali kutumika kisiasa. Huu ni udhaifu wa kitaasisi.

Kitima ameshindwa kuficha maslahi binafsi aliyonayo kwa msingida mwenzie Lissu. Kanisa Katoliki kuendelea kumuacha Kitima kuwa kiongozi wa Kanisa ni udhaifu wa kimfumo dhidi ya kiongozi.

Kwamba Kanisa Katoliki lipo tayari kumlinda kiongozi anayepigania maslahi binafsi kwa kujikinga kwenye ngao ya dini.
Ni uongo kwamba walioenguliwa ni wa upinzani tu?
 
Apewe ujumbe wa kamati kuu Chadema, analichafua kanisa. Kanisa limekubali kutumika kisiasa. Huu ni udhaifu wa kitaasisi.

Kitima ameshindwa kuficha maslahi binafsi aliyonayo kwa msingida mwenzie Lissu. Kanisa Katoliki kuendelea kumuacha Kitima kuwa kiongozi wa Kanisa ni udhaifu wa kimfumo dhidi ya kiongozi.

Kwamba Kanisa Katoliki lipo tayari kumlinda kiongozi anayepigania maslahi binafsi kwa kujikinga kwenye ngao ya dini.
Kuhimiza uwajibikaji, uhuru wa kutoa maoni, kupinga utekaji na kuhimiza chaguzi huru na haki ndiyo maslahi binafsi kwake?
Acha upumbav na kujitoa akili kisa hizo siasa uchwara za kiccm
 
Back
Top Bottom