Padri Kitima: Viongozi wa dini hamuwezi kutenganishwa na siasa na mkiiweka siasa pembeni, mtakuwa hamjaelewa majukumu yenu ya msingi

Padri Kitima: Viongozi wa dini hamuwezi kutenganishwa na siasa na mkiiweka siasa pembeni, mtakuwa hamjaelewa majukumu yenu ya msingi

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Katibu wa baraza la maaskofu katoliki Tanzania (TEC) Padri Dkt. Charles Kitima ameendelea kusisitiza kuwa viongozi wa dini hawawezi kutenganishwa na siasa kwani viongozi hao kuiweka siasa pembeni ni kutokuelewa majukumu ya msingi kama viongozi wa dini.

Akizungumza mkoani Kilimanjaro amesema kinachofanya viongozi hao kuingia katika siasa ni kupeleka tunu walizokabidhiwa na mwenyezi Mungu kutoka kwenye biblia na Quaran huku akisisitiza kuwa siasa zote zilianza katika madhehebu.

Soma pia: Father Kitima: Wizi wa kura ni dhambi, Viongozi wa dini mmekaa kimya!

Video: Jambo TV
 
Katibu wa baraza la maaskofu katoliki Tanzania (TEC) Padri Dkt. Charles Kitima ameendelea kusisitiza kuwa viongozi wa dini hawawezi kutenganishwa na siasa kwani viongozi hao kuiweka siasa pembeni ni kutokuelewa majukumu ya msingi kama viongozi wa dini.

Aidha amesema kinachofanya viongozi hao kuingia katika siasa ni kupeleka tunu walizokabidhiwa na mwenyezi Mungu kutoka kwenye biblia na Quaran huku akisisitiza kuwa siasa zote zilianza katika madhehebu.

View attachment 3161051

Video: Jambo TV
Mafisi yanataka yapewe uhuru wa kurarua wanadamu,kamwe yasiupate uhuru huo.
 
Townchild,
Ningependa kufahamu ikiwa kwa maneno hayo ya Padri Dr. Kitime ni kuwa sasa anaona ni sawa kuchanganya dini na siasa.

Uelewa wangu wa historia toka enzi ya Tanganyika kuchanganya dini na siasa ulikuwa mwiko mkubwa.

Wakati ule wa kupigania uhuru wa Tanganyika ukisikia "kuchanganya dini na siasa," maana yake kwa uhakika bila kutafuna maneno ilikuwa kuchanganya Uislam na siasa.

Inashangaza leo kuwa Katibu wa Baraza la Maaskofu Kanisa Katoliki anataka siasa ichanganywe na dini.

Mwaka wa 1958 Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU Sheikh Suleiman Takadir alifukuzwa TANU kwa kosa la kuchanganya dini na siasa.

Sheikh Suleiman Takadir akapigwa pande na nduguze Waislam na wakampa jina, "Takadir Mtaka Dini."

Sheikh Suleiman Takadir akafutwa katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Mwaka wa 1963 Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti wake Iddi Tulio lilivunjwa na Halmashauri Kuu ya TANU kwa tuhuma za kuchanganya dini na siasa.

Vipi leo kanisa linataka viongozi wake wachanganye dini na siasa?
 
Back
Top Bottom