TANZIA Padri Wilfrid Dinho Wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Afariki Dunia

Pole sana Askofu Ruzoka, Mapadre wenzake na Wakatoliki kwa ujumla wa Jimbo kuu la Tabora. Mungu amrehemu na kumpumzisha pema peponi. Amina.
Alikuwa mtu poa sana huyu padre, roho imeniuma sana. Mwalimu wangu wa kwanza wa Engilish. Kila jioni nilikuwa naenda ananifundisha English pale kwa ma padre. Dah.. imeniuma sana.
 
Ee Mwenyenzi Mungu uipumzisho Roho Baba Padri mahali pema peponi.
Amina
 
Alikuwa mtu poa sana huyu padre, roho imeniuma sana. Mwalimu wangu wa kwanza wa Engilish. Kila jioni nilikuwa naenda ananifundisha English pale kwa ma padre. Dah.. imeniuma sana.
Alikuwa smart sana nami alikuwa mwalimu wangu wa kwanza wa kiingereza akija Mihayo kutufundisha akitokea Itaga Seminary. Alikuwa na utatu mtakatifu na huku akicheza Baisket ball na kuna kipindi alikuwa kocha wa timu maarufu mkoani Tabora zama hizo ikiumana na Uyui. Naizungumzia Mihayo Sec. Ila alikuwa na matatizo ya kiafya kwa muda mrefu sana. Kuna kipindi alikaa sana hapa Dar. R.I.P Dinoh
 
Ameniuma sana, bado naona picha yake inakuja kichwani full, kipe kipindi tunakaa pamoja na kuongea mambo kadha kunifundisha na kunipa moyo na kunijengea moyo wa kujiamini katika uwezo wangu. πŸ˜‘πŸ˜‘
 
Kanisa Katoliki linapaswa kuchukua msimamo thabit kuwalinda walei, watawa na makreli wote.

-Lianze sasa kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya korona bila kukoma na katika taasisi zake zote.
-Kanisa likemee bila uoga upotoshaji wa aina yeyote unaokataa uwepo wa ugonjwa wa korona.
-Kanisa lihamasishe upatikanaji wa chanjo kupitia wafadhiri wake ili kuweza kuyakinga makundi ya makreli, watawa na manesi ambao wako katika hatari kubwa ya kupata maambukizi.
-kanisa liandae mpango wa upatikanaji wa chanjo kwa waumini wake hata kama itakuwa kwa kuchangia gharama.
 
Mungu mpokea mtumishi wako Amen
 
Sawa kabisa,R.I.P Baba Padre
 
Mimi nawashangaa akina Father Kitima, kazi kulaumu serikali tu wakati wao kama kanisa wamechukua hatua gani? wafunge makanisa hadi janga hili lipungue, Italy na Ulaya walifunga.

Hapa nini kinashindikana? Kututajia idadi ya mapadre na ma sister wanaokufa sio suluhisho hata kidogo, kanisa wachukue hatua wao, maana jumuia zinaendelea, mikusanyiko makanisani inaendelea, alafu akifa padre lawama kwa serikali, kwani serikali ndio imewaua? kipi kigumu wasisitishe kanisa kwa miezi kadhaa? Au hawaoni Italy etc
 
mwanga wa milele umuangazie eeh Bwana.πŸ™
 
Padri wa 27.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen
 
Tunashukuru kwa taarifa
 
Kifo hakikimbiliki..!! Kuna mdau hapo kaeleza kuwa alikuwa na matatizo ya kiafya kwa mda mrefu sana...!! So Mungu kaamua kumchukua mja wake.
 
Usiwashangae . Nchi hii tumejiwekea kitanzi sisi wenyewe. Kuna mtu amepewa mamlaka za kimbingu na katiba ya nchi, na jambo lisilompendeza yeye basi inatakiwa wote mlichukie bila kuhoji . Hapo ndipo tulipokwamia
 
Usiwashangae . Nchi hii tumejiwekea kitanzi sisi wenyewe. Kuna mtu amepewa mamlaka za kimbingu na katiba ya nchi, na jambo lisilompendeza yeye basi inatakiwa wote mlichukie bila kuhoji . Hapo ndipo tulipokwamia
Usiishie kumlaumu mtu wakati una nafasi ya kuchukua hatua za kukuponya. Mwaka jana kuna Askofu alisitisha ibada kwenye jimbo lake na Serikali haikumuingilia. Tusilaumu kwa sababu tuna chuki na mtu fulani haitosaidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…