Kwenye hili ni tofauti mkuu,leo asubuhi waziri ametoa statement ya serikali kwa msisitizo kuwa ni marufuku kutangaza hata vifo vya wapendwa wetu,huko mwanzo hatukuwahi kuzuiwa kufanya hivyo,zamani ikitokea tatizo la mlipuko wa maradhi serikali ilitoa taarifa na kusisitiza kuwa kila atakayepata ujumbe huu amwarifu na mwenzake,kwenye hili tunaambiwa hata kama una taarifa kaa kimya!! Usimwambie yeyote,zamani kipindupindu kiliitwa kipindupindu hivyohivyo,na mtu akifa kwa kipindupindu tuliambiwa wazi ili wengine tuchukue tahadhari,leo huruhusiwi hata kutamka neno corona mbele ya wenye mamlaka,toka kitambo tuliambiwa kuwa chanjo ni haki ya kila mtu,ila chanjo ya corona imekuwa haramu kwa nchi yetu tu! Tafakari,na ujue si kila hatua una haki ya kuchukua,hasa ukiwa mtanzania