SI KWELI Pafyumu inaweza kutibu jeraha la kujikata

SI KWELI Pafyumu inaweza kutibu jeraha la kujikata

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwa na dhana ya kwamba ukijikata na jeraha kuanza kutoka damu basi ukipulizia Pafyumu damu inakataa na kidonda kukauka.

Je, kuna uhalisia wowote? Na kwa upande mwengine kuna madhara yeyote kwenye hili?

1712672797283.png
 
Tunachokijua
Pafyumu au uturi ni kimiminika kilicho andaliwa maalumu na kuwekea harufu nzuri. Pafyumu hutumiwa na watu kukabiliana na harufu mbaya au kuondoa harufu mbaya.

Kumekuwa na tabia ya watu kupulizia Pafyumu (Uturi) kwenye kidonda au wanapopata jeraha kwa lengo la kukausha damu na kutibu jeraha.

Upi ukweli kuhusu suala hili?
JamiiCheck imewasiliana na Mtaalamu wa Afya Dkt. Norman Jonas, Daktari na Mkufunzi wa Afya ambaye amekanusha suala la pafyumu (Uturi) kuweza kutibu jeraha. Akiifafanulia Jamiicheck suala hili Dkt. Norman Jonas anasema:

Hakuna uhalisia wowote wa kuwa pafyume inatibu jeraha la kujikata, kufanya hivyo kunaweza kusababisha jeraha lingine.
Dhana hii imetokana na baadhi ya Watu kujua kuwa kuna viambatanishi vingine kwenye pafyumu ikiwemo Alcohol ambayo ni ‘disinfectant’ ambapo inaua bakteria lakini Alcohol iliyopo katika pafyumu sio disinfectant. Disinfectant kitaalam ni kama ilivyo Spirit.
Kuliko kuanza kutumia Pafyumu ambayo ina mambo mengi pamoja na Alcohol ndani yake, tumia maji kuosha kidonda hicho, au usitumie spirit ambayo ni maalum kwa vidonda wewe utumie Pafyumu!
Hivyo, kutokana na ufafanuzi wa Mtaalamu huyu wa Afya hoja inayodai kutumia uturi kunaweza kutibu jeraha haina ukweli.
Back
Top Bottom