Mpendwa Nyamayao... anachokwambia Fidel80 ni kitu kinachotokea sana kwenye ndoa hizi.... Kuna cases nyingi sana za aina hii. Asilimia kubwa sana ya wanaume wanashiriki ngono na ndugu wa wake zao... Wadogo zenu (especially siku hizi) wana tabia za ajabu sana... anapokuona una amani kwenye ndoa yako, anaona kwamba unafaidi sana, anadhani mumeo anakupa kila kitu, mfano gari, pesa, nk. Sasa na yeye anahisi kwamba atafaidi the same way... Kwa hiyo anaanza kujilengesha kwa mwanaume.... na unajua wanaume ni kama panya... hata kama kuna magunia 100 ya mahindi stoo atataka ayatoboe yote ajue kilichomo, kwa hiyo usitegemee (under the sun) kwamba pindi mdogo wako atakapojilengesha mwanaume atamwacha... ni mmoja kati ya 100 atafanya hivyo.
Sasa kumbuka kwamba mpaka mdogo wako afikie kufanya haya atakuwa na ill intentions, anataka kufanya mapinduzi na ujue wanapokuwa kwenye majamboz ndio unakuta na mwanaume anatoa ahadi kedekede... akianza na Blackberry, anaambia mengine yatafuata. Kumbuka mwanaume anakuwa anamtumia tu kama kiburudisho, lakini mdogo wako yeye anakuwa na ill intentions za kumiliki... then inatokea Mimba.... U know the rest...
Lakini kumbuka pia ni vigumu sana kwa mwanaume kuzuia tamaa zake especially akiwa na binti karibu yake, mara kavaa kipedo, mara kaptula na kitopu sijui, mara nightdress nyepesii anawatakia usiku mwema, mara kanga moja, kwa kweli jamaa atafanya kila hila mpaka ampate... Msaada wa Mungu unahitajika sana katika hili.... Dumuni katika maombi