Paji la uso na siri ya jicho la tatu

Mshana naomba unifahamishe kuhusu THIRD EYE CHAKRA na binaural meditation maana niliviona youtube lakini sikuweza kuvielewa.
Ni kitu kile kile kwa mtazamo tofauti zote mbili ni kuamsha nguvu za asili zilizolala ni sawa na kwenye martial arts kuna kung-fu karate tai-chi nk
 
ni kweli ukiactivate (ukiROOT ubongo) third eye unaweza kuwaona majini na wachawi?
Kwenye high level si hivyo tuu bali viumbe vyote visivyoonekana kwa macho ya kawaida na unaweza kufanya mengi ambayo binadamu wa kawaida hawezi fanya
 
Mshana naomba uendelee na mada hii nafikiri bado unavitu vya kuongeza khhusiana na paji la uso.. Ningependa kujifunza zaidi
Haina shida lakini sasa mwendelezo utakuwa ni kwa mtindo wa kujibu maswali
 
Kwenye high level si hivyo tuu bali viumbe vyote visivyoonekana kwa macho ya kawaida na unaweza kufanya mengi ambayo binadamu wa kawaida hawezi fanya

Kuna video nmetizama Youtube inasema Mungu amekataza kufungua third eye coz anajua kuwa utapofungua kuna negative spirits utaziskia,zitakuposess na kukuaminisha kuwa wewe sasa ni mkuu zaidi ya Mungu maana una uwezo wa kuona/kusikia vitu visivyoskika kwa hali ya kawaida ya kibinaadam hivyo unauwezo wa kujiunga na dini inayoendana na ulimwengu huo (illuminati),na pia ni rahisi sana kuingiliwa na Majini/mashetani na kukutumia vile watakavyo, Pia hii ishu ya third eye watu wa Illuminati ndo wanacheza nayo sana hata nembo yao inawakilisha third eye so kwa maana hiyo jamaa kasema (you do at your own risk) kinyume na hapo utakua umekwenda tofauti na matakwa ya mwenyez Mungu

NB: nlitaka njaribu ila baada ya kupitia maoni ya watu huko youtube waliofungua jicho hilo nimeghairi ghafla!. wanasema utapofungua kulifunga itachukua muda mrefu so utaishi kwa hofu sana
 
Mkuu, niliwahi kujaribu hii kitu mwaka juzi baada ya kusoma post za watu humu. Nilijaribu kama kwa siku mbili tatu hv nakumbuka hiyo siku kichwa kiliniuma sana pia natetemeka kila saa, nilikuwa na machale hv yaani nilikuwa kwenye hali flani ambayo nashindwa kuiandika. Mfano niliweza kugundua kuna mtu yuko nje ya mlango wangu kasimama, ilihali alikuja kimya. Kuna vitu vingine sivikumbuki, niliogopa na nikaacha ku- meditate. Mkuu mshana, nilipatwa na kitu gani
 
Duu kwanini ukaacha? Ulikuwa unaenda vizuri sana
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Mkuu Mshana mbon ile link nimefata inaonyesha hakuna kitu? Niilienda pia Google engine search nikasearch sioni pia. Nataka link itakayonipeleka nisome jinsi ya kumeditate ambayo umeandika wewe.
 
Mhhh so bro jicho la tatu ni sawa sawa na macho ya rohoni? If Yes bas hata pia kuna sikio la Tatu ambalo ni sikio la ndani( sikio la kiroho)

If all above ni kwel bas yatupasa kumtafuta Mungu kwa bidii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…