Paka akiondoka panya hujitawala, haya huu ni wakati wa panya na ukoo wake kufurahia soka bila uwepo wa YANGA, kunawatu wamepigwa chenga ya mwili.

Yaani mashuti na kosa kosa nyingi walizokuwa wanapiga Yanga kama sio uimara sa kopa wa APR Yanga angeshinda goli nyingi halafu mtu anasema Yanga hawakuhitaji haya mashindano.
 
Yanga hawachelewi kusema APR waliingia na mapanga uwanjani.
 
Kwenye matokeo haya maelezo sijayaona pamoja na kutafuta kwa juhudi.
Nilichokiona ni hiki
APR 3 - Yanga 1
 
Nakubaliana na wewe , kwa kuongezea hizi bonanza huwa zinachosha sana wachezaji na majeraha wakirudi Kwenye mashindano lazima wachemke nafuu Hata bonanza lenyewe liwe la ela nyingi kama AFL .
Angalia wydad walivyokuja kuchoka ndiyo maana vilabu vikubwa ulaya havitaki bonanza !
 
Una uhakika yanga walimpa masharti ya kuchukua bonanza la mapinduzi katika mkataba wake ?
Ili yanga ipate kipimo kizuri icheze na timu iliyojuu yake caf kwa maana ya Al ahly , Mamelodi au zinazokaribia Kama raja , tp Mazembe , pyramid , espirance, na sio vinginevyo hapo ndiyo kocha ataweka first eleven yake au Hilo shindano liwe na donge Nono .
Kuweka kambi yenyewe kwa siku sio chini ya milioni 5 Mpaka 10 halafu zawadi milioni 100 na timu unazocheza nazo zipo rank ya chini .
Sasa umuumize mchezaji muhimu kwa bonanza la kitoto si itakuwa kukosa maarifa wakati kuna makombe makubwa yapo mbele.
 
Umeshindwa kumuelewa, amemaanisha kama Gamondi angekuwa ana lengo la kushinda, angepanga wachezaji wengi waliohusika kwenye kipigo cha goli tano cha Simba yaani Pacome, Aucho, Yao, Max, wasingekosekana.
 
Hiyo yote ni kwa sababu Yanga kafungwa
 
kwa hapa naweza kusema umeongea pumba
 
Panya ndo wamekimbia mashindano kisa uwepo wa paka
 
wenye akili tutaishi humo,makolo kutoka sehemu mbalimbali dar walifanya party na kukesha jana...jamaa wanaishi dunia yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…