Paka wa Kenya agundulika kuwa na Virusi hatari aina ya FIV, vinavyofanana na virusi vya UKIMWI

Paka wa Kenya agundulika kuwa na Virusi hatari aina ya FIV, vinavyofanana na virusi vya UKIMWI

Ni matokeo ya kulawiti wanyama, sasa wafanye utafiti kwa PUNDA, MBWA, BATA, na KUKU, MBUZI maana hawa jamaa ni kiboko.

Tuna subiri Dr alete mrejesho
 
Kumbe Paka/wanyama wana Uraia/Nationalities siku hizi..........au ndio yale ya Vyura wa Kihansi??!!
 
Hii ni dawa ya kuwapunguza kura za mumbis experts wa kuwalawiti wanyama!
 
PAKA.jpg


Kwenye nchi ya Kenya virusi hatari aina ya FIV vinaavyofanana kabisa na virusi vya HIV vinavyosababisha UKIMWI vimegunduliwa katika paka mmoja ikiwa ni baada ya uchunguzi wa kina wa damu ya paka huyo kuthibitisha uwepo wa viini vinavyofanana kabisa na vile vinavyoathiri binaadamu.

Wafugaji wa paka na wanyama wa nyumbani wametakiwa kuwapeleka wanyama wao kufanyiwa uchunguzi wa afya wanapowashuku wanyama wao wanaugua, virusi hivyo vinaitwa FIV (Feline Immunodefficiency Virus) na wanasema ugonjwa huu sio mgeni kwa wanyama.

kwa mujibu wa BBC SWAHILI, Mwaka wa 1986 madaktari wa Marekani waligundua virusi vilivyofanana kwa karibu na vile vinavyoambukiza binadamu vya HIV lakini hii ndio mara ya kwanza kwa virusi hivyo kugunduliwa nchini Kenya.

Madaktari wa maabara ya Lancet Nairobi waligundua kuwa virusi hivyo vinasababisha ukosefu wa kinga mwilini na kudhoofisha afya ya wanyama hao wanaopendwa na kuishi majumbani lakini hata hivyo waliwahakikishia wafugaji wa paka kuwa hakuna ushuhuda wowote wa maambukizi kutoka kwa paka hao kwenda kwa binadamu.

Daktari Dhaval Shah badala yake amewashauri wafugaji wa paka kuwafungia paka wao ndani ili kuwazuia wasijamiiane na wale paka wanaorandaranda mitaani ambao huenda wameambukizwa UKIMWI wa paka ambao unaambukizwa kupitia mate na mkwaruzano paka wanapopigana.
 
Back
Top Bottom