Paka wakamata panya wanauzwa

Paka wakamata panya wanauzwa

Hakika. Mamaa huwa anataka kutoka nje. Akalitafuta na kulipata...
Mkuu kama huko uliko kuna biashara nzuri, basi tunaweza kuingia mkataba niwe nakuagizia paka wa kutosha kwa njia ya basi kila wiki/mwezi!!

Maana huku hatununui! Tunapewa tu bure na majirani! Ukitaka wadogo, wakubwa, majike tu, au madume tu, yote yanapatikana.
 
From lawyer to mjasiria mali muuza paka!!! Ama kweli vyuma VIMEKAZA 😂😂😂😂😂
Paka wenye umri wa miezi miwili ambao ni wa asili na wakamata panya mahiri wanauzwa. Wako watatu. Kila mmoja ni shilingi elfu arobaini. Wanapatikana Survey hapa Dar es Salaam. Wale wote mnaokabiliwa na tatizo la panya majumbani mwenu hapa Dar na kwingineko wahini hii fursa ya kumaliza tatizo lenu.

Mawasiliano ni yangu binafsi kwa njia ya PM.

Nyote mnakaribishwa!
 
From lawyer to mjasiria mali muuza paka!!! Ama kweli vyuma VIMEKAZA 😂😂😂😂😂
😁😁😁😁 Nyinyi si mnatusema kwamba Watumishi wa umma hatujiongezi kufanya biashara na shughuli za ufugaji ili kujiongezea kipato!! Sasa tumeamua kuanza na biashara ya PAKA!!

Tena wewe ni shabiki wa Simba unatakiwa ununue wa kuingia nae uwanjani wakati wa mechi za kimataifa za timu yako.
 
Washawamaliza hao panya naanza kuwapa menu..., au wakati wanawakamata hao panya menu inahusika ?
 
Hivi kuna paka anayepambana na panya miaka hii?

Naona kama watu wamegeuza nyau kuwa viumbe wa kuranda randa ndani tu...
 
Back
Top Bottom