From Chugga
New Member
- Aug 22, 2021
- 4
- 9
Nilipopata akili nilisimuliwa kuwa wazazi wangu walifariki nikiwa mdogo sana. Baba alitangulia na baadae Mama. Walezi wangu wakawa babu na bibi ambao ni wakulima kijijini Manda.
Siku moja, nikiwa darasa la tatu walipita wageni nyumbani ambao walikuja kwa shughuli zao pale kijijini. Walisikia kuhusu habari ya vifo vya wazazi wangu na kuona hali ya pale nyumbani kwetu, wakajitolea kunisomesha.
Siku chache baadae akaja mtu kunichukua, anaitwa Kaka Idd, akanipeleka Jijijni Dar ambako nilitafutiwa shule shule ya English Medium. Nikahamia kwa darasa la nne, kwa sharti kuwa nijitahidi kupata alama nzuri kwa sababu shule niliyotoka ilikuwa ni ya kawaida.
Huko shule mpya nikakutana na watoto kutoka familia zilizojiweza, wakitembelewa na kuletewa zawadi kila weekend. Kaka Idd alinifanya nisijione tofauti, mara nyingi alikuwa ananitembelea na kuniletea vitu nilivyohitaji na zawadi. Actually, alikuwa ndiye pekee aliyekuja kunitembelea pale shuleni wengine walikuwa busy na shughuli zao.
Nikiwa darasa sita, likizo ya mwisho wa mwaka sikurudi kijijini, nikaenda kukaa kwa Mama Mkubwa, Mburahati. Mama Mkubwa alikuwa akisafiri mara nyingi kwa sababu ya shughuli zake na aliposafiri tulibaki wenyewe, yaani mimi na watoto wake ambao hatukupishana sana umri.
Moja moja pakawa na ngoma jirani, Mama Mkubwa hakuwepo nyumbani, tukapata mwanya wa kwenda kuangalia hiyo ngoma.
Nilisimama pembeni ya duka lililokuwa karibu na eneo la shughuli. Kaka wa dukani akaniita, akaniuliza jina, nikamtajia. Akaniambia maneno mengi, kuwa niingie dukani kwake, angenipa pesa, pipi na soda na vitu vingine. Mwanzo nilikataa, lakini alipozidi nikamkubalia kwa ahadi ya kwenda kesho yake.
Siku iliyofuata yakatokea yakutokea nikapoteza usichana wangu na miezi sita baadae Mama mkubwa aliitwa shuleni, akakabidhiwa nirudi nae nyumbani. Nikafutwa shule kwa sababu iligundulika nilikuwa na mimba.
Maisha yakashika mkondo tofauti, sikumuona kaka Idd wala kusikia habari zozote kutoka kwake. Mama Mkubwa akasema hawezi kukaa nami, ikabidi nirudishwe kijijini Manda. Habari kijijini ikawa ni "kapelekwa mjini kusoma karudi na mimba"! Nikawa natolewa mifano kwa wengine nikatajwa hata kwenye sherehe za kumaliza shule, wakaambiwa “msiwe kama waliopata nafasi kupelekwa kusoma wakaurdi na mimba”.
Baadae nikaja kusikia kuwa Kaka Idd aliposikia nimefukuzwa shule alijitahidi kwa kushirikiana na watu wa haki za binadamu kutafuta namna nifanye mtihani wa Taifa lakini hawakufanikiwa, hadi afisa elimu aligoma kusaidia kwa vile sheria ilibana.
Hatimaye siku ambayo wenzangu waliingia kufanya mtihani wa Taifa ndio mimi niliingia leba kujifungua, nikiwa na miaka 12. Sitasahau Bibi alivyokuwa akinisaidia, siwezi hata kuelezea ila yeye na babu ndio walisimama kunishika huku wakiendelea na kazi zao za shamba.
Taratibu nikazoea maisha mapya, nikawa sasa naweza kwenda nje hata kutembea japo bado watu walikuwa wakinisema na mara zingine niliona vidole vikinielekea.
Siku moja, bila kutarajia Kaka Idd akapita kwetu akiwa na shughuli zake, akanikuta tayari nina mtoto. Mwanzo niliona aibu kuonana nae, nilihisi machozi kila nikimuangalia. Ila hakuonyesha hasira au hisia zozote mbaya kwangu……..nakumbuka tu alisema angejitahidi nirudi shule.
Tumaini jipya likaja, nikapata nafasi kidato cha kwanza Jitegemee, nikarudi kukaa Mburahati kwa Mama Mkubwa na Kaka Idd akinipatia mahitaji ya shule na nauli. Nikaahidi ningesoma kwa juhudi zote. Kweli nikaanza vizuri.
Ila jamani Shetani ana nguvu sana, na ana njia nyingi za kufanya kazi yake. Rafiki niliowapata shuleni hawakuwa na u-serious wa masomo kabisa, ikawa ni viduku na muziki. Habari zao mara nyingi zilikuwa za wavulana, tamthilia, story za udaku na fasheni.
Rafiki zangu wawili wakaacha shule kidato cha tatu kwa sababu ya mimba, mmoja aliacha kwa sababu alisumbuliwa na majini ambayo hayakutaka asome. Mimi nilimaliza kidato cha nne lakini matokeo yangu yalikuwa mabaya.
Nikarudi tena nyumbani, mwanangu muda huo ana miaka minne, mwanzo haikuniumiza kichwa sana kwa sababu bibi na babu walibeba jukumu la kupatikana kwa chakula nyumbani. Lakini ilipofika muda mtoto anapaswa kuanza chekechea akili ikanikaa sawa, nikaanza kuhisi uhalisia wa mambo.
Ikabidi kuhangaika kutafuta kazi, nikapata kazi ya kuuza duka la nguo. Mshara ulikuwa mdogo, Boss nae alikuwa mkali, mara nyingi anagomba bila hata sababu. Ikawa inabidi tu nivumilie. Nilipotaka kusimulia hali ile akili ilikuwa ikinisuta, nayameza kimyakimya.
Nikajitahidi kumuhudumia mwanangu, ila hali ilipozidi kuwa ngumu ikabidi nikawatafte wazazi wa kijana yule aliyenipa mimba. Ilikuwa ndio mara ya kwanza kuonana nao, huyo muhusika mwenyewe sikuwahi hata kujua alienda wapi, nilisikia tu alishikwa, lakini aliwekewa dhamana akatoroka.
Mtoto akachukuliwa na bibi yake mzaa Baba, nikabaki mwenyewe kupambana na maisha. Kila mara nakumbuka nafasi ya kusoma niliyoichezea kwa sababu za kipuuzi. Nikajiona mjinga sana, nikakonda sana kwa mawazo na kutokuwa na matumaini au raha ya maisha.
Siku moja tena nikapata taarifa Kaka Idd ananitafuta, na haikuchukua muda nikapata simu kutoka kwake. Akaniuliza nilichokuwa nafanya, nikamsimulia yote. Akaniuliza kama ningependa kusomea ujuzi wowote utakaoniwezesha kupata ajira ya uhakika.
Nilishukuru sana, nikapata nafasi kusoma Veta, mambo ya hoteli. Hapa sasa akili yangu ikakaa sawa, nikasoma vizuri. Nikawa miongoni mwa wanafunzi bora mwanzo hadi mwisho.
Kaka Idd akanitafutia kazi kupitia rafiki yake na ndio kazi ninayofanya hadi sasa. Nashukuru maisha yanaenda na naweza kumsaidia mwanangu na bibi na babu pia.
Kuna nyakati huwa natafakari maisha yangu na nyakati nilizopitia najikita nalia sana, maana katika maisha unaweza kuzungukwa na wengi lakini wasione umuhimu wa maisha yako, akatokea mmoja akakushika mkono kila unapoteleza. Huyo ni zaidi ya malaika.
Nadhani dunia sasa inahitaji wakina Kaka Idd wengi zaidi na kila msichana anahitaji kuwa na kaka Idd wake maisha ya wasichana wengi yangebadilika na huenda kungepungua idadi ya wanaoingia kujiuza au kufanya biashara za ajabu kama pombe za kienyeji na miraa.
Ninachoweza kuwaambia jamii ni kuwa haisaidii sana kusema tu wasichana waepuke vishawishi, kwa sababu wao ni dhaifu na wepesi kuangukia vishawishi vya maneno ya hadaa ya vijana na wanaume. Hivyo kelele pia ipigwe kwa wanaume na vijana waache kuwatia wasichana kwenye vishawishi. Wawaache mabinti wakue na wasome, badala ya kuwatumia kwa haja zao za kimwili na kuwaachia wahangaike wenyewe na mimba.
Halafu, kwa wanaume wanaowapa mimba wasichana na kuwatelekeza, natamani ningeweza kuelezea jinsi msichana anahisi akisikia mtu aliyempa mimba amemkataa. Unahisi dunia yote imekuelemea, tena unaweza usihisi kitu akili ikashika ganzi. Ndio sababu wengine wanaishia hata kujiua, maana kwa wakati huo unachoona ni kiza tu.
Hivi kwanza kwa nini kumfata binti ambaye unajua ni mwanafunzi, unamuona na sare za shule kabisa unajua ikitokea kushika mimba atafukuzwa shule? Anayefanya hivi anatofauti gani na shetani? Maana anakuwa ameharibu maisha ya mtu kwa sababu yakutimiza haja zake za muda mfupi. Mbaya zaidi ni kiumbe kitakachozaliwa, akikuwa anakutana na simulizi kuwa baba yake alimkataa na ndoto za mama yake zilikatishwa na huyo huyo baba yake.
Hali hii kwa nini ipo huku kwetu tu? Mbona kwa wenzetu wazungu tunaona kwenye muvi na tamthilia wanajitahidi kujali maisha ya watoto kwa kiasi kikubwa, hata kama kijana hana kazi akijua msichana wake ana mimba anajitahidi apate kazi kumuhudumia huyo msichana na mtoto atakayezaliwa. Huku kwetu mtu akisikia mimba akili ya kwanza anawaza kula mbio! Najua si wote na nawapa heshima wale wanaokubali majukumu yao, angalao, ingawa lililo bora zaidi ni kuwaacha wasichana wasome kwanza.
Nilisoma kuwa watoto wanaokuwa kwenye mazingira haya huwa wanakuwa na shida za kiakili, wanajiona kuwa hawakutakiwa huku duniani kwa kukataliwa na mzazi wake. Wanawezakuwa na historia ngumu ya ukuaji na kujiingiza kwenye matukio mabaya kama utumiaji wa madawa na uhalifu. Watahitaji uangalizi mzuri ili waweze kukua vema.
Narudia kuwasihi wanaume, tafadhali waacheni mabinti wasome, na mjitolee kuwasaidia mkiona wanaingia katika njia zisizo sawa. Saidieni kusema na vijana wadogo wakware ambao wanadanganyana kwenye makundi ya mitaani.
Na hapa ni muhimu kusema kuwa hata watoto wa kiume wanahitaji sana kupata elimu ya uzazi na jinsia badala ya kuchukulia vitu hivi kimzaha kama ilivyo sasa. Wao ndio wanasababisha zaidi matatizo kwa wasichana kwa kiasi kikubwa.
Kama una binti au ndugu wa kike, tafadhali, muwalinde na kuwaongoza vema. Huenda wanakutana na vishawishi vingi. Najua mara nyingine tunakuwa wagumu kupokea ushauri lakini huo ndio wakati tunahitaji kuangaliwa kwa njia zote, hata maombi.
Muhimu jamii na familia kuelewa mabadiliko ya tabia kutokana na umri wa balehe, kwa sababu hiki ni kipindi wengi hawakilewi. Wanaishia kuwalalamikia wamekuwa jeuri kumbe ni kwa sababu tu ya kipindi cha umri wanachopitia.
Ukiweza kumsaidia binti yoyote ambaye amekatisha masomo kwa sababu ya mimba au sababu nyingine yoyote ile, fanya hivyo. Utakuwa umemuokoa yeye na kizazi chake.
Serekali kupitia vitengo husika itafakari namna ya kuwasiaidia wasichana waliokatisha masomo kwa sababu yoyote ile, ili kuwawezesha kujikimu, kuhudumia watoto wao na kupunguza idadi ya watu tegemezi katika jamii. Bado wanaweza kufundishika na wakapata taaluma za kuwasaidia na hata kuwa na msaada mkubwa kwenye jamii kwa kuwafundisha wengine.
Walimu wanaweza kuwa msaada mkubwa kwa wasichana wanapokuwa karibu nao, wanaweza kugundua mabadiliko ya tabia na dalili zakuwa wanapitia changamoto kwa sababu ya taaluma zao. Hivyo waongeze ukaribu na watoto wa kike kutumia vema nafasi yao ya ulezi.
Kwa kumalizia niseme si sawa hata kidogo kuwasema vibaya wasichana wanaokatishiwa masomo na mimba, kwa sababu hiyo mimba ni mzigo wa mateso tayari, kumuongezea mingine wanaweza kuelemewa na kuishia kupata msongo wa mawazo au kuchukua maamuzi ya kutoa mimba na kujiua. Zile kauli za “si alidhani ni pipi, hakuju kama tamaa mbaya” hazina maana kabisa na zinaweza kupelekea matokeo mabaya zaidi kwa wasichana husika.
Ukiona dereva boda, daladala, muuza chipsi, muuza duka au mwingine yeyote yule anamzengea mtoto wa shule, tafadhali chukua hatua, japo kuongea utakuwa umesaidia.

Upvote
3