Pre GE2025 Pakifanyika Reforms kwenye Katiba kupata Tume huru ya Uchaguzi, Watanzania wanaweza kuiamini na kuipigia kura CCM, tuondoe hofu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
mzee Kikwete aliishia njian baada ya kugundua mambo yanaweza kugeuka, ni wakat wa Kikwete ndio kulikuwa na idadi kubwa ya wabunge wa upinzani, hii ilihatarisha kuleta hofu chamani, ndio maana Magufuli akataka kufuta kabisa
 
Watz Wana moyo wa shukrani sana,

Hawawezi kuikataa CCM ikiwa itahakikisha Tume huru ya Uchaguzi inapatikana, Sanduku la kura linaheshimika, maoni Yao yanasikiwa!!
 
mzee Kikwete aliishia njian baada ya kugundua mambo yanaweza kugeuka, ni wakat wa Kikwete ndio kulikuwa na idadi kubwa ya wabunge wa upinzani, hii ilihatarisha kuleta hofu chamani, ndio maana Magufuli akataka kufuta kabisa
Wanadai Mzee Kikwete alidhamiria,

Ila wahafudhina ndani ya chama ndio walioingilia kuharibu.

CHADEMA Haina mizizi ya kutosha kuiangusha CCM Kwa ghafula, labda huko 2030.
 
Tangu mwaka uanze, leo ndo nimesoma uzi wenye akili kutoka kwa mwana CCM
 
CCM Imechaguliwa na wananchi uchaguzi wa mwaka 2005, chaguzi zote zilizofuatia waliiba.
 
Watachaguliwa na nani au watachaguliwaje? Dogo mbona swali jepesi hili?

Kwani hujui jinsi Tume huru za uchaguzi ambavyo huwa zinapatikana kwenye mataifa mengine?

Kiufupi ni kwamba wadau wa uchaguzi hupewa nafasi ya kupendekeza majina watu huru wasioshikamana na chama chochote. Kisha kutoka kwenye majina hayo, taasisi huru kama vile viongozi wa dini, asasi zisizo za kiserikali, vyama vya kitaalama, wanawapigia kura.
 
CCM Imechaguliwa na wananchi uchaguzi wa mwaka 2005, chaguzi zote zilizofuatia waliiba.
Si Kweli,

Kuengua wagombea Majimboni kulififisha matumaini ya wananchi kushiriki uchaguzi na kuchagua viongozi wawatakao.

Ije tu Tume huru ya Uchaguzi.
 
Ajitoa ufahamu huyu mtu.

Na jambo hili Si geni,Tulishalianza tangu huko awali na sasa ni la kuimalizia tu.

Uzuri Mzee Warioba mwana CCM yupo Bado.
 
Tangu mwaka uanze, leo ndo nimesoma uzi wenye akili kutoka kwa mwana CCM
CCM Ina njia nyingi za kushinda uchaguzi hata ikiwepo hiyo Tume huru ya Uchaguzi na Katiba mpya,

Bado Wana machinery za kushinda vita ya Uchaguzi.

CCM inaweza kubadilika na kupokea mabadiliko haya na kuendelea kusalia mamlakani Kwa HAKI.
 
Ccm haichukiwi sabbu inaharibu uchaguzi, inachukiwa kwasababu imeshindwa kutatua kero za Watanzania
 
Ahahahahaha! Mtu akikaa kimya sio rahisi kugundua kuwa ni mpumbavu! Ahahahahaha!!
 
Unawapanga wajae ee 🀣🀣🀣
 
Ccm haichukiwi sabbu inaharibu uchaguzi, inachukiwa kwasababu imeshindwa kutatua kero za Watanzania
Sasa kero za wananchi zinatokana na viongozi wanaojixhagua Kwa kura fake.

Huoni uhusiano hapo juu?

Kwamba kinajisiwa Sanduku la kura ni chanzo Cha matatizo yote yanayowakumva Watanzania?

CCM ukubali HOJA hii na tuvuke mkwamo huu Kwa Amani kama alivyofanya Kikwete kuruhusu mchakato wa Katiba mpya!
 
Hapabadilishwi hata nukta wala koma kwa makelele ya kibaka au mtu mwingine yeyote .

CCM itashinda uchaguzi kwa zaidi ya 98% Oct 2025, please note that πŸ’
 
Wanadai Mzee Kikwete alidhamiria,

Ila wahafudhina ndani ya chama ndio walioingilia kuharibu.

CHADEMA Haina mizizi ya kutosha kuiangusha CCM Kwa ghafula, labda huko 2030.
wakijichanganya hiatasubiri mizizi mkuu, 2015 Dar yote ilikuwa Chadema ikabidi zifanyike juhudi za makusudi, maana mzee wa Chato ilibidi ahamie Dodoma, ndio ukasikia zile habari ya kuunga juhudi zikaanza, mara ukonga, mara kinondon na kwingineko
 
Unawapanga wajae ee 🀣🀣🀣
Wapi wewe,

CCM imewahi kujichunguza yenyewe na kutamani kujivua gamba ,na walifanikiwa Kwa kiasi Fulani,

CCM ilileta vyama vingi ambapo wananchi hawakuvitaka,

Sasa kuruhusu Tume huru ya Uchaguzi Kwa kubadili Katiba ni jambo dogo Hilo.
 
Wapi wewe,

CCM imewahi kujichunguza yenyewe na kutamani kujivua gamba ,na wakifanikiwa Kwa kiasi Fulani,

CCM ilileta vyama vingi ambapo wananchi hawakuvitaka,

Sasa kuruhusu Tume huru ya Uchaguzi Kwa kubadili Katiba ni jambo dogo Hilo.
Gamba liliishia kichwani mkuu halikutoka,
 
wakijichanganya hiatasubiri mizizi mkuu, 2015 Dar yote ilikuwa Chadema ikabidi zifanyike juhudi za makusudi, maana mzee wa Chato ilibidi ahamie Dodoma, ndio ukasikia zile habari ya kuunga juhudi zikaanza, mara ukonga, mara kinondon na kwingineko
Alisikika shujaa Magu akisalimia Pipoooz!

Akacopy agenda za upinzani ikiwemo ujenzi wa reli ya sgr,

CCM ikaendelea kuongoza,

HOJA zijibiwe Kwa HOJA, Si kutekana,

Hawa washamba wanaoingiza HOFU CCM iogope mabadiliko,hawaitakii mema!
 
Umeongea pumba mdau hiyo katiba mpya ya kikwete iko wapi? Uchaguz serikal za mitaa nafikiri ni wewe ndo hukuelewa kilichoendelea na zile fomu za matokeo hukuziona my take CCM inashinda chaguz kwa goli la maradona kila uchaguz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…