Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Hili taifa miaka yote tangu kuanzishwa kwake huwa liko katika migogoro ya kisiasa.
Mawaziri wake wakuu rasmi wote 18 waliowahi kuingia madarakani hakuna aliyewahi kumaliza awamu yake ya uongozi.
Lazima moja kati ya kuuwawa, kupinduliwa, kuondolewa kwa kura ya kutokuwa na imani au kujiuzulu na kukimbia ofisi mwenyewe!
Imran Khan waziri mkuu maarufu sana nayo yamemkuta hayo hayo na sasa jeshi linataka kumpiga pini asirudi kwenye siasa tena.
Marais wake wote nao ilikuwa hivyo hivyo kama yaliyowakuta mawaziri wakuu kabla ya kupunguza madaraka ya Ofisi ya Rais na kumfanya kuwa ceremonial tu mwaka 2010.
Jeshi na Idara ya Usalama ya Taifa wanapewa billion za dola kila mwaka na Marekani kupambana na ugaidi ila wako na misuguano kila wakati na Marekani kwamba hawafanyi kazi yao na badala yake wanaotoa hifadhi kwa magaidi wengi. Uhusiano ulikuwa mbaya zaidi ilipokuja kugundulika Osama Bin Laden alikuwa anaishi umbali wa nusu maili tu kutoka chuo kikuu cha jeshi la Pakistan na Marekani wakafanya operation ndani ya nchi yao bila kuitaarifu serikali ya Pakistan.
Pakistan pamoja na kuwa taifa la kidini ndio kitovu cha biashara ya Opium inayolimwa Afghanistan ambayo inayotumika kutengeneza dawa za kulevya za Heroin na Morphine.
Wao pia kama majirani zao na mahasimu wao India wanamiliki silaha za nuclear pamoja na kuwa ni taifa la hovyo sana.