Pakistan yaanzisha sheria ya uhalifu inayolenga ukosoaji mtandaoni

Pakistan yaanzisha sheria ya uhalifu inayolenga ukosoaji mtandaoni

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Serikali ya Pakistan imeanzisha sheria mpya ya uhalifu wa mtandaoni ambayo inaweza kuwafanya watumiaji wa mitandao ya kijamii kufungwa hadi miaka mitano jela kwa kuchapisha "habari za kughushi " kuhusu jeshi, mahakama au maafisa wa umma.

Sheria hiyo iliidhinishwa na baraza la mawaziri la Waziri Mkuu Imran Khan na kupitishwa haraka kuwa sheria na Rais Arif Alvi.

Hata hivyo wakosoaji wanasema sheria hiyo ni sehemu ya hatua za kubinya uhuru wa kujieleza katika taifa hilo.

Tume ya Haki za Kibinadamu ya Pakistan, imeitaja sheria hiyo kuwa kinyume cha kidemokrasia.

Adhabu ya juu pia imeongezwa kutoka miaka mitatu hadi mitano na watuhumiwa hawatapewa dhamana, kwa maana hiyo mshitakiwa atasubiri kusikilizwa kwa kesi yake gerezani. Muungano wa Shirikisho la Wanahabari wa Pakistan umeapa kupinga marekebisho hayo mahakamani.

DW
 
I hope nape na Makamba jr wanashughulikia kurekebisha kale kasheria kakiboya.
 
Back
Top Bottom