Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Mamlaka ya udhibiti wa vyombo vya habari vya utangazaji ya Pakistan, PEMRA, imezipiga marufuku televisheni nchini humo kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mkutano wa waziri mkuu wa zamani Imran Khan aliopanga kuufanya hii leo.
Marufuku hiyo ilitolewa jana jioni, ikiwa ni siku ambayo Khan alifanya mkutano mjini Islamabad. Khan alitumia mkutano huo kuwakosoa maafisa wa polisi na mahakama juu ya kukamatwa kwa mmoja wa viongozi wa chama chake.
Serikali imesema katika katazo lake kwamba Khan anatoa madai yasiyo na msingi na kueneza kauli za uchochezi. Tangu aondolewe madarakani kupitia kura ya kutokuwa na imani naye, nyota huyo wa mchezo wa Kriketi amefanya mfululizo wa maandamano ya kuipinga serikali.
Khan anatarajiwa kufanya mkutano mwingine leo jioni katika mji jirani na Islamabad.