Pakistani yashambuliwa na kikundi cha wanamgambo kutokea Ndani ya Nchi, wanajeshi 14 wapigwa kombola wakiwa ndani ya gari

Pakistani yashambuliwa na kikundi cha wanamgambo kutokea Ndani ya Nchi, wanajeshi 14 wapigwa kombola wakiwa ndani ya gari

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Baloch Liberation Army (BLA) imekiri kuhusika na mashambulizi mawili mabaya dhidi ya vikosi vya jeshi la Pakistan huko Balochistan, yaliyosababisha vifo vya wanajeshi 14, wakiwemo maafisa wa ngazi za juu. Katika tamko kali, BLA imeapa kuongeza operesheni zake, ikilitaja jeshi la Pakistan kuwa kundi la mamluki linalohudumia maslahi ya mataifa ya kigeni.

Baloch Liberation Army (BLA) ni kikundi cha wanamgambo wanaopigania kujitenga kinachofanya kazi hasa katika eneo la Balochistan nchini Pakistan. Kikundi hiki kinatafuta uhuru wa eneo la Balochistan linalopatikana kusini mwa nchi hiyo ya Pakistan, kikidai kuwa unyonyaji wa kiuchumi, kutengwa kisiasa, na ukandamizaji wa kitamaduni unaofanywa na serikali ya Pakistani ndiyo sababu za harakati zao. BLA ni mojawapo ya vikundi kadhaa vya kitaifa vya Baloch vinavyoendesha harakati za kijeshi katika eneo hilo na kimeorodheshwa kama kikundi cha kigaidi na Pakistan, Marekani, na Uingereza.

Pakistan hiki kipindi wanapitia wakati mgumu baada ya kupata mashambulizi kadhaa kutoka jeshi la India na Sasa kikundi cha BLA kikiipiga Pakistan kutokea ndani ya Nchi.

 
Back
Top Bottom